Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (katikati)akipatiwa maelezo juu ya uzalishai kutoka kwa Meneja uzalishaji Mgodi wa SUNSHINE GROUP Ndugu Lusajo Mwakabungwe.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipitia taarifa ya Mgodi

Godlove Mwamsojo Mratibu wa NEMC kanda ya Nyanda za juu Kusini akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla juu ya utunzaji wa mazingira kwa wewekezaj hao ambapo kikubwa amewataka wawekezaji kuhakikisha  wanaisaidiaserikali katika  kufuata msharti waliopewa na baraza la mazingira NEMC.

Eneo la Mgodi wa SUNSHINEGROUP Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi wa SUNSHINE wakiendelea na shughuli za Uchimbaji mgodini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika Mkutano na wananchi wa Itumbi kusikiliza kero za wananchi na kutatua mgogoro uliopo kati ya wananchi na mwekezaji Vicent Minja Mkazi wa Dar es salaam,ambapo hivi karibuni kulitokea maafa kwa watu 4 kupoteza maisha wiki moja iliopita hali iliyofanya Mkuu huyo wa Mkoa kusitisha zoezi la uchimbaji mgodini hapo sanali na kuagiza  Kamati ya Ulinzi wilaya, kamishina wa madini, mwekezaji, uongozi wa kata, kitongoji na wawakilishi 5 wa wananchi kukaa kwa pamoja kupata muafaka
Pia amemwagiza kamishina wa madini kufuta leseni za wataoshindwa kuendeleza na maeneo hayo wapewe wachimbaji wadogo
Huku akimtaka  kamishina wa madini kukagua migodi na kuangalia usalama wa migodi 
Wananchi wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa Mkoa Amos Makalla Itumbi Wilayani Chunya.

Mkutano ukiendelea.....

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top