Bondia
Floyd Mayweather ameweka rekodi katika ulimwengu wa ngumi baada ya
kushuka ulingoni mara 50 bila kupoteza hata pambano mara moja.
Rekodi hiyo mpya ameiweka leo (Agosti 26 kwa saa za Marekani) baada ya
kumdhibiti Conor McGregor ambaye alikuwa ni hasimu wake katika pambano
lililokuwa likisubiriwa kwa hamu katika mzunguko wa 10 na kufanikiwa
kuibuka na ushindi wa alama 87 dhidi ya 84 za Conor.
McGregor alianza vizuri pambano hilo kwa kumtwanga Mayweather lakini
baadae kibao kilimgeukia huku akitupiwa makonde na kushindwa kujibu.
Baada ya pambano hilo lililofanyika katika uwanja uliopo Las Vegas,
Mayweather amesema kuwa Conor ni mpiganaji mzuri kuliko alivyodhania
lakini ameweza kuwapa mashabiki wake na wapenzi wa ngumi, kile
walichokuwa wakikisubiria kwa hamu.
Mayweather amesema kuwa hilo lilikuwa ni pambano lake la mwisho na ana
uhakika kwamba alichagua mshindani mzuri (Conor) ambaye alimpa ushindani
mkubwa.
Hapa chini ni baadhi ya picha kutoka kwenye pambano hilo;
Post a Comment