Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akisisitiza jambo
mbele ya Waandishi wa Habari(hawapo pichani) alipokuwa akizungumzia
uhusiano wa matumizi ya tumbaku na magonjwa ya moyo jana Jijini Dar es
Salaam.
……………………………………………………………………………………
Picha na: Frank Shija -MAELEZO
Na Agness Moshi – MAELEZO.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) imetoa taadhari kwa watumiaji wa sigara kujiepusha na matumizi
ya sigara kwasababu wapo kwenye hatari ya kuugua magonjwa ya Moyo yanayo
sababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu.
Akiongea na Waandishi wa Habari
kwenye mahojiano maalum Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa
JKCI Prof. Mohamed Janabi amesema ni vyema wananchi kujiepusha na
utumiaji wa sigara kwa sababu moshi unapoingia kwenye moyo huaribu na
kuziba mishipa inayopitisha damu kwenye Moyo na hivyo kuusababisha
kushindwa kufanya kufanya kazi yake vizuri.
“Moyo umezungukwa na mishipa ya
damu ambayo inauwezesha kufanya kazi endapo mishipa hii itaharibiwa na
moshi wa sigara,damu inayozalishwa kutoka kwenye moyo itakua chache na
hivyo kusababisha mtumiaji kupata matatizo ya moyo kama vile mshituko
wa moyo, kushindwa kupumua vizuri kutokana na kubanwa kwa mishipa ya
damu”,alisema Prof.Janabi
Prof.Janabi amesema kuwa, kwa
kawaida Moyo wa binadamu kila unapopiga unatakiwa uzalishe milita 70
ambapo kwa mapigo 70 ni sawa na mililita 4900 ambazo ni sawa na lita 5
kwenye mwili wa binadamu ikitokea mishipa ya damu imezibwa damu
itazalishwa kwa uchache hivyo kusababisha mtu kuvimba miguu, kushindwa
kupanda ngazi au sehemu za miinuko na kupata maumivu makali kama
amechomwa na kisu.
Prof.Janabi ameongeza kuwa kuziba
kwa mishipa ya kupitisha damu kwenye moyo hakuuathiri Moyo tu bali
mwili mzima ikiwa ni pamoja na ubongo, hivyo inapotokea mishipa hiyo
imezibwa kunahaja ya kutafuta njia ya kusaidia damu ipite vizuri kwenye
moyo kwa kupandikiza mishipa mingine ambayo itatolewa kwenye sehemu
nyingine za mwili kama kwenye miguu na mikono au kwa kumuwekea mgonjwa
chuma ambacho kitasaidia damu kupita vizuri.
Prof.Janabi alisema kuwa, gharama
zinazotumika kwa ajili ya kusaidia mishipa iliyoharibiwa ni kubwa
ukilinganisha na faida mtumiaji wa sigara anayoipta kutokana na utumiaji
wa sigara kwa sababu vifaa vyenyewe viavyotumika ni ghali, gharama za
uchunguzi na matibabu, pia muda wa kumuokoa ni muhimu kuzingatiwa
endapo mgonjwa ameathirika sana.
“Kama mishipa ya damu imebana kwa
asilimia 90 au 100 Mgonjwa anatakiwa afike Hospitalini ndani ya lisaa
limoja na nusu endapo atachelewa hakuna kitakachoweza kufanyika zaidi ya
Kifo unaweza ukawa na uwezo lakini muda hautakuruhusu”,alisisitiza
Prof.Janabi.
Aidha, Prof.Janabi amesema kuwa
,tatizo la uvutaji wa sigara nchini si kubwa sana ukilinganisha na Nchi
za magharibi japo linakua kwa kiasi kwenye miji mikubwa ambapo watu
watumiaji na watu wanaokaa karibu na mtumiaji kwa muda mrefu
wanaathiriwa na Moshi unaotokana na sigara ambapo athari zake huonekana
kwa nyakati tofauti.
“Wagonjwa wengi tunapokea hapa
wanakua na sababu nyingine kama uzito mkubwa,Kisukari na presha na kwa
uchache tunapokea wagonjwa wanaumwa kwa sababu ya matumizi ya sigara kwa
wingi ,unakuta wanatumia pakiti moja hadi tatu kwa siku pia mara nyingi
tunapowafanyia uchunguzi wa awali wagonjwa ni ni lazima tuwaulize kama
wanatumia sigara kwa sababu sigara ni moja ya kisabishi cha ugonjwa wa
Moyo”, alisema Prof.Janabi.
Hata hivyo, Prof.janabi ametoa
wito kwa Wananchi kuhakiksha wanapima Afya zao mara kwa mara ili waweze
kugundua matatizo mapema kabla hayajaleta na madhara makubwa kwenye
mwili pia amewataka watumiaji wa sigara kujiepusha na matumizi ya sigara
kwani madhara yake ni makubwa.
Post a Comment