WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekipiga marufuku Chuo Kikuu Ardhi kukodi makampuni ya kufanya kazi mbalimbali kwa niaba yake.
Amesema
kitendo hicho kinaharibu kazi na sifa ya chuo hicho kwa kuwa baadhi ya
makampuni wanayoyapa kazi hayakidhi vigezo.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo
leo (Alhamisi, Novemba 23, 2017) kwenye ufunguzi wa sherehe za
maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu Ardhi.
“Kama
kuna umuhimu wa kufanya kazi na kampuni ni bora muanzishe kampuni ya
kwenu itakayofanya kazi vizuri ili kujiepusha na matatizo.”Pia Waziri
Mkuu amekiagiza chuo hicho kufanya tafiti zenye kuleta majibu ya maswali
na changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa na Dunia.
Ametaja
baadhi ya changamoto hizo kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi, ujenzi
holela, uharibifu wa mazingira na majanga ya asili kama mafuriko.Amesema
Serikali inaamini kuwa matokeo ya kazi zinazofanywa na chuo hicho
zikiwemo tafiti ni chachu ya maendeleo ya taasisi za elimu ya juu.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa imeweka
mkazo wa kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kupato cha kati ifikapo
2025, hivyo wanahitajika wataalamu wa kutosha na wenye weledi.“Hivyo
Chuo Kikuu cha Ardhi kama taasisi ya Serikali inawajibu mkubwa wa
kutayarisha wataalamu mbalimbali wa sekta za ujenzi, ukadiriaji majenzi
na uhandisi wa mazingira.
Pia
Waziri Mkuu amewataka watumie fursa hiyo ya kuadhimisha miaka 10 ya chuo
hicho kujitafakari na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuwekeza zaidi
ili kuongeza tija ya uwepo wa taasisi hiyo kwa jamii na Taifa kwa
ujumla.“Wekeni mikakati madhibuti itakayowezesha chuo kupiga hatua kubwa
zaidi katika kipindi cha miaka 10 ijayo. Siku zote mjikite katika
kutafuta kuwa na ubora zaidi ya wakati uliopita.”
Awali,
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
alisema Serikali inakkitegemea chuo hicho katika kufanikisha ajenda yake
ya uchumi wa viwanda kwa kuwa kinatoa wataalamu wengi.
Maadhimisho
hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya, Mwenyekiti wa Baraza la chuo Bibi Tabitha Siwale,
Makamu Mkuu wa chuo Profesa Evaristo Liwa pamoja na viongozi mbalimbali
wa Serikali, wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, NOVEMBA 23, 2017.
Post a Comment