Mamlaka ya usalama wa uchukuzi nchini Kenya NTSA imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi.
Madereva
walevi sasa watalazimika kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia
maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za barabarani.
''Hatuwezi
kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya ajali na wanapofikishwa
mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha kutengeza sera hiyo
mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria'', alisema mkurugenzi wa mamlaka
hiyo Francis Meja.
Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini. CHANZO BBC
Post a Comment