Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye
ni Naibu Waziri wa kilimo akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa
wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye
ni Naibu Waziri wa kilimo akimvalisha kofia ya CCM kijana aliyehama Chadema wakati wa kampeni za Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa
wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye
ni Naibu Waziri wa kilimo akifurahi na wananchama wa CCM wakati wa mkutano wa kumnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa

Na Mathias Canal,
Mbeya
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye
ni Naibu Waziri wa Kilimo amewasihi wananchi kwa kauli moja kuchagua kiongozi
makini anayetokana na CCM.
Mhe Mwanjelwa
alisema kuwa kumchagua diwani wa CCM ni dalili nzuri ya kumpongeza na kuunga
mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli anazozifanya kwa muktadha wa kuwaletea maendeleo watanzania
wote.
Mjumbe huyo wa
NEC, aliyasema hayo Leo Novemba 20, 2017 katika Mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Kijiji cha Bujinga A na B kilichopo Kata ya Ibigi, Wilayani Rungwe Mkoa
wa Mbeya ambapo alimnadi mgombea Udiwani wa Kata hiyo Bi Suma Ikenda Fyandomo.
(Mnec), Mhe
Mwanjelwa aliwakumbusha wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kuwa
Hawachagui ilani mpya Bali wanachagua Diwani kwa ajili ya kutekeleza ilani ya
Ushindi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 ambayo wananchi waliiamini na kuichagua
Octoba 25, 2015.
Alisema kuwa
nchini Tanzania hakuna chama chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi Bali
Chama Cha Mapinduzi pekee ndicho chenye uwezo na jukumu la kuwaletea maendeleo
endelevu wananchi.
Katika Mkutano huo
wanachama 21 walivutiwa na hotuba ya Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM
wakati akimnadi mgombea hivyo kufanya maamuzi ya kujivua uanachama wa CHADEMA
na kujiunga na CCM ambapo wameahidi kushirikiana na mgombea udiwani wa CCM ili
kuhakikisha anashinda kwa kishindo.
Ushiriki wa
kampeni hizo katika Kata ya Ibigi unajili wakati ambapo Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine
Kesho Disemba 21, 2017 atashiriki ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Tawala na
washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini juu ya mfumo wa ununuzi wa
mbolea (BPS).
Mkutano huo
utafanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa Jijini Mbeya.
MWISHO
Post a Comment