Afisa
Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto)
wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kusaini makubaliano
rasmi na Benki ya TPB ambapo sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale
wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha
kulipia kidogo kidogo. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB,
Sabasaba Moshingi pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Multichoice
Tanzania, Salum Salum.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto)
wakisaini makubaliano ya ushirikiano, ambapo kwa sasa wafanyakazi umma,
wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa
mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Nyuma yao ni mashahidi kutoka
pambe zote mbili.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kusaini
makubaliano rasmi na kampuni ya Multichoice Tanzania inayotoa huduma za
DStv, sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja sasa
wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo
kidogo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage
Chande.
BENKI
ya TPB imeingia kwenye makubaliano rasmi na kampuni ya Multichoice
Tanzania inayotoa huduma za DStv ambapo wafanyakazi umma, wateja na hata
wale wasio wateja sasa wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na
kisha kulipia kidogo kidogo.
Hafla
hiyo ya kusaini makubaliano imefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande wamesaini
hazi za makubaliano.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi alisema kwa sasa Watanzania
wanaotaka kumiliki ving’amuzi vya DStv, wataweza kupata mkopo maalum
kutoka TPB utakaowawezesha kufungiwa huduma za DStv na kisha kulipa kwa
awamu kwa kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja.
Alisema
kuwa benki yake siku zote imekuwa ikijitahidi kubuni huduma mbalimbali
kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kupata huduma muhimu na
pia katika kuboresha hali zao kiuchumi na kijamii.
Amesema kuwa wameamua kuingia kwenye makubaliano na kampuni ya Multichoice ili kuwapa fursa wafanyakazi na wateja wa benki hiyo waweze kupata huduma muhimu za DStv kwa mkopo, hii ikimaanisha hawatalazimika kulipa fedha yote kwa mkupuo mmoja badala yake watakuwa wanalipa kwa awamu kadhaa.

“Benki
yetu ni benki ya Watanzania wa kada zote, na wenzetu wa Multichoice nao
hali kadhalika, sasa tumeamua tuungane ili tuwawezeshe ndugu zetu
Watanzania kupata fursa ya kuwa na huduma ya DStv kwa njia ambayo ni
rahisi kwao” alisema Moshingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande aliishukuru TPB kwa kukubali kuwawezesha watanzania kupata huduma za DStv kihimiza wananchi kuitumia vema fursa hiyo. Alisema huduma za ving’amuzi vya DStv ni bora nchini Tanzania hivyo urahisishaji wa wananchi kuipata unaongeza wingo wa wananchi kufurahia huduma hizo.

Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Post a Comment