Na Teresia Mhagama.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa TANESCO
kuhakikisha kuwa hawakati Umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea
wananchi adha ya kukosa nishati hiyo.
Naibu
Waziri aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa TEDAP
unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme
ambapo vituo vya kupozea Umeme alivyovitembelea ni Mbagala, Gongo la
Mboto, Kipawa na City Centre.
“Umeme
ukatike pale inapostahili tu, na endapo tatizo linatokea mfano kwenye
mifumo ya Umeme ni muhimu mkatoa taarifa mapema kwa wananchi,” alisema
Subira Mgalu.
Aliongeza
kuwa ukatikaji wa Umeme unasababisha malalamiko kutoka kwa Wananchi
kwani kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli nyingi hasa za
kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato.
Aidha
Naibu Waziri aliwaagiza watendaji wa TANESCO wanaosimamia mradi huo wa
TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika
tarehe 15 Desemba, 2017.
Vilevile
alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri na kwamba
kukamilika kwake kutaboresha hali ya upatikanaji wa Umeme katika jiji la
Dar es Salaam.
"Nawaomba
watanzania wawe na matumaini na Serikali ya Awamu ya Tano kwani
inajitahidi katika Ujenzi wa miundombinu ya Umeme, nia ikiwa ni nishati
ya Umeme kupatikana muda wote," alisema Naibu Waziri.
kwa
upande wake, Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka
TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manirabona alisema kuwa Shirika hilo
linafanya juhudi mbalimbali ili utekelezaji wa mradi huo ukamilike ndani
ya muda ulioelekezwa.
Mradi
wa TEDAP unahusisha upanuzi na ujenzi wa Vituo Vipya 19 vya kupoza
Umeme wa Msongo wa kV 132/33 na kV 33/11 pamoja na ujenzi wa njia za
Umeme wenye Msongo wa kV 132, kV 33 na kV 11 katika Mikoa ya Arusha, Dar
es Salaam na Kilimanjaro.
Gharama
za utekelezaji wa mradi husika ni Dola za Marekani milioni 43, ambazo
zimetolewa na Benki ya Dunia (WB) kupitia Mradi huo.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa kwanza kushoto) akiwa katika eneo
la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi
wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar
es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji
Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manirabona.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akikagua mitambo ya
Umeme katika kituo cha City Centre jijini Dar es Salaam wakati
alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na
ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha ni
watendaji kutoka TANESCO.
Baadhi
ya mitambo ya Umeme katika kituo cha Mbagala jijini Dar es Salaam
iliyojengwa chini ya mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa
njia za Umeme jijini Dar es Salaam.
Miundombinu
ya kusafirisha Umeme wenye Msongo wa kV 132 iliyojengwa katika eneo la
Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa
uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akikagua mitambo ya
Umeme katika kituo Kipawa jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara
ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za
Umeme jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha ni watendaji kutoka
TANESCO na Wizara ya Nishati
Post a Comment