Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa
jimbo la Nzega,Dkt Hamisi Kigwangalla,ambaye pia ni Waziri wa Maliasili
na Utalii mapema leo mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi ndani ya
jimbo la Nzega.kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee
Hassan Wakasuvi pamoja na Katibu wa CCM Wilaya Ndugu Shaibu Ngatiche.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mbunge wa
jimbo la Nzega,Dkt Kigwangalla,mapema leo walipokuwa wakishuhudia ngoma
ya asili iliyokuwa ikitumbuiza nje ya Ofisi kuu ya chama ya wilaya ya
Nzega mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi kufuatia mwaliko wa Mbunge
wa jimbo hilo Dk Hamisi Kigwangalla.kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ndani ya Ofisi
kuu ya chama ya wilaya ya Nzega na kuitambulisha kamati kuu ya siasa
ya Wilaya mapema leo kabla ya kwenda kwenye mkutano wa ndani wa jimbo
hilo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mbele ya Kamati kuu ya
Siasa Wilaya ya Nzega,mkoani Tabora mapema leo,mara baada ya kupokea
taarifa fupi za chama ndani ya Ofisi kuu ya chama ya wilaya hiyo
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda na viongozi wengine wa chama
wakielekea kuweka jiwa la msingi la ujenzi wa Ukumbi utakaotumika kwa
shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii,liliojengwa kando kando ya Ofisi kuu ya chama ya wilaya
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uwekaji
rasmi wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ukumbi mkubwa na wa kisasa
utakaotumika kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii,uliojengwa
kando kando ya Ofisi kuu ya chama ya wilaya hiyo,kulia kwake ni Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo
Dkt Hamisi Kigwangalla (aliyevaa mawani katikati).
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo
Dkt Hamisi Kigwangalla wakipiga makofi mara baada ya kuwekwa jiwe la
msingi la ujenzi wa ukumbi .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na Katibu wa CCM Wilaya Ndugu Shaibu Ngatiche wakikagua ujenzi wa ukumbi huo . PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mapema leo mbele ya
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Nzega mkoani Tabora.Ndugu
Kinana amefanya ziara wilayani humo mapema leo kwa Mwaliko wa Mbunge
wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii
Dkt Hamisi Kigwangalla,aidha katika ziara hiyo Ndugu kinana amewapongeza
viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika ngazi ya chama ya wilaya na
pia kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa ambao
utatumika kwa matumizi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na Wananchi wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo wilayani Nzega mkoani
Tabora.Ndugu Kinana amewasili Wilayani humo kwa ziara fupi ya Mwaliko wa
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na
Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,aidha katika ziara hiyo Ndugu kinana
amewapongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika ngazi ya chama ya
wilaya na pia kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa ukumbi mkubwa wa
kisasa ambao utatumika kwa matumizi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
Ndugu
Kinana akiagana na baadhi ya Wananchama wa CCM waliofika kumpokea
katika Makao Makuu ya Ofisi ya Wilaya hiyo mapema leo mchana.Ndugu
Kinana anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa jimbo la Nzega katika
mkutano wa ndani wa jimbo hilo jioni ya leo.
Post a Comment