Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)Bi. MarieHellen Minja, wakishuhudia tukio la utiaji saini wa mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini, Mhandisi Patrick Mfugale, akibadilishana nyaraka za mkataba mara baada ya kusaini na Mkandarasi wa Kampuni ya Jiangxi Geo Bw. Chen Xianghua leo jijini Dar es salaam,  atakayejenga barabara ya Usesula hadi Komanga km 108.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipokea zawadi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kama ishara ya shukrani kwa ajili ya ujenzi wa barabara jimboni kwake, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji saini mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bi. MarieHellen Minja, mara baada ya kushuhudia  tukio la utiaji saini wa mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay zenye jumla ya (kilomita 402), jijini Dar es Salaam.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top