Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


January 3, 2017 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei mpya elekezi za Mafuta ya Petrol, Diesel pamoja na mafuta ya Taa kwa Mwaka. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia January 3.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, bei zitakazoanza kutumika leo Petroli imezidi kupanda bei kwa shilingi 8/lita, kupanda huku kumetokana na mabadiliko ya bei katika soko la Dunia.

Pamoja na kutaja bei kikomo za bidhaa mbalimbali za mafuta nchi nzima, EWURA wametaja mambo muhimu ya kuzingatia nakusogezea kama walivyotoa katika taarifa yao ya leo kama ifuatavyo.
  • Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Kwa mwezi Januari 2018, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 8/lita (sawa na asilimia 0.35), Shilingi 34/lita (sawa na asilimia 1.71) na Shilingi 89/lita (sawa na asilimia 4.57) sawia. Vilevile, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 7.56/lita (sawa na asilimia 0.37), Shilingi 33.97/lita (sawa na asilimia 1.81) na Shilingi 88.73/lita (sawa na asilimia 4.85) sawia. Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji (BPS Premiums).
  • Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Bei za Mafuta ya Taa hazijabadilika kwa sababu hakuna Mafuta ya Taa yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga katika mwezi wa Disemba 2017. Katika toleo hili, bei za rejareja za Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini zimeongezeka kwa Shilingi 60/lita (sawa na asilimia 2.78) na Shilingi 69/lita (sawa na asilimia 3.47), sawia. Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 59.68/lita (sawa na asilimia 2.93) na Shilingi 69.02/lita (sawa na asilimia 3.67). Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli na Dizeli katika mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji (BPS premiums).
  • Ifahamike kwamba, sehemu kubwa ya shehena za mafuta yaliyopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam ni zile zenye bei za soko la dunia za mwezi Oktoba 2017 wakati shehena iliyopokelewa katika bandari ya Tanga ni ya bei za soko la dunia za mwezi Novemba 2017. Bei za mafuta katika soko la dunia kwa mwezi Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya asilimia 6 ikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2017.
  • Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika, zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.
  • Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top