Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha
Hazina, Bw. Eligius Mwankenja alipokua akifungua mkutano wa mwaka wa Chama
hicho Jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa chama hicho kinatoa riba ya kiasi cha asilimia 6.5 hadi 9 ilihali Taasisi
nyingi za Fedha zikiwemo Benki hutoa riba ya zaidi ya asilimia 20 jambo
linalochangia ongezeko la Mikopo chechefu.
“Hazina
Saccos kwa kutambua kuwa watu wanaokopa wengi hawana dhamana kama nyumba, ardhi
na vingine, imeamua kutumia kigezo cha kubakiwa na 1/3 ya mshahara kama kigezo
cha kupatiwa mkopo wenye riba nafuu” alifafanua Bw. Mwankenja.
Kwa
upande wake Meneja wa Hazina Saccos ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Chama hicho
Bw. Festo Mwaipaja, alisema kuwa chama hicho kipo chini ya Wizara ya Fedha na
Mipango na kinahudumia Wafanyakazi wa Serikali na taasisi zake.
Kutokana
na uwezo mkubwa wa chama hicho kujiendesha kimetoa ajira kwa wafanyakazi 11
ambao wanatekeleza majukumu ya kila siku ya chama na pia kimekuwa kikipata
faida na kutoa kodi kwa Serikali hivyo kuchangia katika pato la Taifa kwa
ujumla.
Aidha
Chama kinatarajia kufungua mradi mkubwa wa Kitega Uchumi maeneo ya Njedengwa
Mkoani Dodoma kwenye eneo lililotengwa kwa ajili yauwekezaji zikiwa ni juhudi
za kukuza mtaji na kuchangia maendeleo.
“Jambo
linalo vutia katika chama hichi ni kuwa Mwanachama wa Hazina Saccos anaweza
kuchangia Sh. 20,000 kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu lakini akawa na uwezo
wa kukopa zaidi Sh. milioni moja hadi milioni tatu pia tunatoa mikopo ya
biashara kwa wanachama jambo ambalo ni suluhisho la mitaji hivyo kuchangia
kukuza uchumi wa nchi”. alieleza Bw. Mwaipaja.
Vilevile
kimetoa viwanja kwa bei nafuu katika maeneo ya Kigamboni kwa Sh. 6500 kwa mita
ya mraba, Chasimba kwa Sh. 4000, Kiluvya Sh. 7500 na sasa kinatarajia kutoa
viwanja Mkoani Dodoma katika Maeneo ya Ihumwa, Ngaroni na Nzuguni B.
Chama
cha Hazina Saccos kilianzishwa mwa 1973 kikiwa na wanachama 250 lakini kwa sasa
Chama hicho kina wanachama hai 5045.
Post a Comment