Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameitwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa sababu isiyojulikana.
Wawili hao wamesema wanahisi wito huo unatokana na mkutano wa hadhara alioitisha mbunge huyo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Sugu amesema leo Jumanne kuwa, juzi jioni alipigiwa simu na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) kwamba yeye na Masonga wafike jana ofisini kwa ajili ya mazungumzo lakini alimueleza kuwa itakuwa ni siku ya sikukuu hivyo itakuwa vigumu ngumu kwenda, hivyo walikubaliana wafike leo.Chanzo Dar 24

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top