Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

TUESDAY, JUNE 5, 2018

TUESDAY, JUNE 5, 2018

MAkamu wa Rais azindua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais wa ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.  Ni muhimu, mipango ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kazi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira unahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote. Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika India katika mji wa New Delhi yakibeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati Mbadala”

Mapema leo, Makamu wa Rais alizindua ukuta wa bahari uliopo kwenye barabara ya Barack Obama wenye urefu wa mita 920, ukuta huo ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi kavu unakadiriwa kuwa na maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa. Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda na zipo faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na Tanzania kuwa na Viwanda.

Mwisho, Makamu wa Rais amesema katika kufanikisha suala zima la uhifadhi wa Utunzaji wa mazingira mi lazima tuifanye kila siku iwe siku ya Mazingira. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ukuta wa bahari wenye urefu wa mita 920 uliojengwa pembezomi mwa barabara ya Barack Obama mara baada ya kuizindua, mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Bw. Leonard Kushoka mfano wa hundi yenye thamani ya shiliningi za kitanzania milioni 300 mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa mwaka 2018, wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mwenyekiti Mkazi wa Kampuni ya Shell Bw. Axel Knospe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisisitiza jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January  Makamba, akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikagua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam mara baada ya kuuzindua mapema hii leo, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Sehemu ya kupumzika iliyojengwa katika ukuta wa ufukwe wa bahari ya Hindi uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Msanii Beka Fleva akitoa burudani kwa wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,(hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wananchi mara baada ya kuzindua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Picha na Eliphace Marwa – MAEL

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

  1. How To Find Out How To Play Slots For Real Money And Win Real
    It is quite 제천 출장마사지 simple to 전라남도 출장마사지 pick 전라북도 출장마사지 up and place an online 군포 출장마사지 slot machine online, and so the machine becomes a real money option to make 바카라 money. For example,

    ReplyDelete

Top