Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MONDAY, JUNE 4, 2018

WATANZANIA WATAKIWA KUJIUNGA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA

Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Dennis David akimpima mkazi wa Jiji la Tanga Octaviani Moshiru kwenye banda lao  lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifaDaktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Dennis David akimpima mkazi wa Jiji la Tanga Octaviani Moshiru kushoto akimsikiliza kwa umakini mkazi wa Jiji la Tanga Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza akimpa ushauri mkazi wa Jiji la Tanga mara baada ya kupima afya.Katibu tawala mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akipima afya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Hillary Ngonyani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kushoto ni Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Korogwe Jumanne Shauri kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa DuguzaMkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Jumanne Shauri kushoto akisaini kitabu cha wageni kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa DuguzaMkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Jumanne Shauri kushoto akizungumza na maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata kushoto ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa Duguza
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens kulia akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika kwenye banda lao kupata elimu ya mpango wa kujiunga na bima ya AfyaKatibu Tawala wa mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akiwa na tisheti akijiandaa kuwapa watoto zawadi wakati alipotembelea banda hilo kushoto Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu sehemu ya watoto waliojiunga na mpango wa Toto Afya kadi




NA MWANDISHI WETU, TANGA.


WATANZANIA wametakiwa kujiunga na mpango wa bima a Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu ya uhakika wakati wanapokuwa wakiugua na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuingia gharama kubwa.

Hayo yalisemwa leo na Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hawa Duguza wakati akizungumza kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya biashara ya kimataifa.

Licha ya mfuko huo kutoa elimu juu ya umuhimu wa mpango wa bima lakini pia wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa afya na kutoa ushauri kwa wananchi ambao wamekuwa wakifika kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesha hayo.

Alisema mpango wa bima ni mzuri kutokana na kuwapa uhakika wa matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali na hivyo ni muhimu kujiunga nao ili waweze kuona manufaa makubwa wanayoweza kuyapata.

Aidha pia aliwahamasisha kujiunga na mpango wa kikoa na toto Afya kadi ambazo ni muhimu kwa ajili ya kuweza kupata huduma nzuri kipindi ambacho wanapatwa na changamoto za kuugua hususani watoto wadogo wakati wa ukuaji wao.

“Ndugu zangu maradhi huwezi kujua yanakuja lini hasa kwa watoto wadogo wakati wa ukuaji wao hivyo niwasihi muone njia nzuri ya kuwawekea akiba ya matibabu kwa kuwaingiza kwenye mpango huu wa toto afya kadi kwani hii ni kumuhakikisha mtoto wako huduma wakati wote wanapougua”Alisema.

Alisema pia jamii haiwezi kupata maendeleo ikiwa watakuwa hawana afya bora hivyo ni muhimu kuendelea kuhamasishana kujiunga na mpango huo kwa lengo la kuweza kunufaika na huduma za matibabu (habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top