Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelezo ya nyaraka zilizoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka kwa Mkurugenzi wa mifuko ya Uwezeshaji (NEEC), Bw.Edwin Chrisant wakati wa maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Nzovwe Mbeya Oktoba 20, 2018 |
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa maonesho hayo. |
Na EmanuelMadafa,MichuziBlog,Mbeya
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC) kufanya tathamini ya wananchi walionufaika na mikopo
iliyotolewa kwenye Taasisi za kifedha ili kubaini idadi halisi ya wananchi hao.
Ametoa
kauli hiyo hii leo (Oktoba 20, 2018) wakati akifungua maonesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya
Nzovwe Mbeya ambapo yalijumuisha wajasiliamali kutoka Wilaya 15 za Mikoa ya
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Amesema
Lengo la kufanya tathimini hiyo ni kupata uhalisia wa wanufaika wa mikopo hiyo
ili kuenenda sambamba na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekusudia
kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.
Aliongezea
kuwa, tathimini hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya
Serikali yao hususani wenye mtizamo hasi kuwa serikali haijafanya jambo lolote
kuwawezesha kiuchumi.
“Tathimini
hii itasaidia kuwa na utaratibu mzuri wa kutunza takwimu sahihi zinazoonesha
uhalisia wa wanufaika pia italeta chachu kwa kuhakikisha maonesho haya
yanafanyika kwa mzunguko na kutoa fursa kwa wananchi wengi hasa maeneo ya
vijijini kufahamu mifuko na programu za uwezeshaji nchini”.Alisitiza Mhagama
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa aeleza kuwa
ofisi yake itaendela kutekeleza kwa vitendo eneo la uwezeshaji wananchi
kiuchumi na kuyachukua maagizo ya waziri ili kuhakikisha malengo yaliyoainishwa
yanafikiwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mhe.Albert Chalamila alipongeza juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu
kuhakikisha wananchi wote wanawezeshwa kiuchumi na kujikwamua katika hali za
umasikini na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.
“Lazima tuendelee kuunga mkono
jitihada za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vitendo na kuhakikisha changamoyo ya ajira
kwa vijana inakomeshwa na kuwa na Taifa lenye maendeleo na wananchi
wake”.Alisema Chalamila.
Aidha,
kaulimbiu ya maonesho ya Mwaka huu inasema “Vikundi vya Kifedha,
Programu na Mifuko ya Uwezeshaji ni Chachu ya Maendeleo ya Viwanda”.
=MWISHO=
Post a Comment