Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kocha Msaidizi wa Mbeya city Ndugu Maka Mwalwisi akizungumza na Blog hii juu ya tetesi za yeye kuachana na Mbeya Mbeya Msimu huu

Na EmanuelMadafa,Mbeya

Zikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa msimu Mpya wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara Timu ya Mbeya  City Fc inayoshiriki Ligi hiyo huenda wakanza vibaya kutokana na kuondokewa na Kocha Msaidizi wa Timu hiyo .

Taaria za kuondoka kwa Kocha zilianza kuenea katika maeneo mbalimbali katika jiji la Mbeya hali ambayo iliiradhimu blog hii   kumtafuta kocha huyo ili kuweka bayana juu ya yeye kuondokana na Timu hiyo.

Akizungumzia sakata hilo Kocha huyo Msaidizi wa Mbeya City Maka Mwalwisi,amesema kitendo cha yeye kuendelea kukinoa kikosi hicho ni kujifungia uwezo na ujuzi wake wa kufundisha hivyo wakati umefika  wa kutafuta timu nyingine na kuiendeleza.

Aidha amebainisha wazi kuwa  mkataba wake ndani ya Mbeya City ulimalizika Mei 30 mwaka huu ambapo katika kipindi hicho alifanikiwa kupata nafasi ya kwenda kupata mafunzo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na CAF na kufanikiwa kupata lesseni daraja B.

Amesema, mafunzo hayo ambayo  makubwa nchini Tanzania kwa makocha yamechangia yeye kufanya maamuzi ya kupima uwezo wake kwa kutafuta timu ambayo ataanza nayo kuanzia ligi daraja la kwanza mpaka hapo itakapofikia.

Amesema, kila kocha anapoishika timu na kuifundisha hutumia ujunzi na uwezo wake hivyo kitendo cha yeye kuendelea kubaki Mbeya City ni kufungia ujuzi  wake kabatini.

Aidha, Kocha Maka amewaomba mashabiki kuendelea kuipa ushirikiano timu ya Mbeya City kwani anaamini ya kwamba timu hiyo ikiwa na kikosi chake kile kile itaendelea kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Aidha Maka amesema kuwa changamoto anayoiona mbele ya timu hiyo ni hatua ya wachezaji kuwa mbali nay eye kwani amekuwa na wachezaji kwa muda mrefu kabla ya hata kujiunga na mbeya city.

Amesema kuwa kikubwa ambacho wachezaji hao watakikumbuka kwa kocha huyo ni hatua ya kuwaweka karibu na kuondoa tofauti zao pamoja na kuwaanda vyema kukabiliana na changamoto za kimchezo na maisha ya kimpira kwa ujumla wake.

Hata hivyo, hakusita kummwagia sifa kocha Juma Mwambusi ya kwamba ni mwalimu mzuri huku akiupongeza uongozi wa timu nzima ya Mbeya City kwa kuwa na utaratibu mzuri wa uendeshaji wa timu kwani mpaka sasa anachokifahamu ni kwamba timu hiyo haijatoa mchezaji nje bali inatarajia kuingiza wachezaji.

Wakati huo amewataka wapenzi wa Timu hiyo ya Mbeya City pamoja na wadau kwa ujumla kutoa weka fikra zozote mbaya juu ya yeye kuondoka mbeya city badala yake waione kama sehemu tu changamoto katika harakati za kimchezo
Mwisho.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top