Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Tanesco Mkoa wa Mbeya Bw.Cyprian Lugazia akiwa katika moja ya majukumu yake ya kukamata wahujumu wa shirika hilo.

Na EmanuelMadafa,
WANAWAKE wawili wanashikiliwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mbeya, kwa tuhuma za kuhusika na uuzaji na usambazaji wa mafuta ya Transfoma.

Wanawake hao, ambao ni wakazi wa eneo la Ilomba lililopo Jijini Mbeya, walikamatwa jana majira ya saa mbili usiku, wakiwa na lita 10 za mafuta hayo, wakitafuta wateja wa kuwauzia.

Kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Tanesco Mkoa wa Mbeya,Cyprian Lugazia aliwataja wanawake hao kuwa ni Grace Jeremia maharufu kwa jina la (Mama Matha) ambaye ni muuzaji mzoefu na Sera Zakaria.

Aidha, Afisa huyo, amesema watuhumiwa hao walikutwa na madumu hayo mawili ya lita tano  kila moja  na kuwa mpaka sasa maofisa wa shirika hilo wanaendeleza msako mkali dhidi ya watu wengine ambao wamekuwa wakilihujumu shirika hilo na kusababisha hasara kubwa kwa serikali.

“Watuhumiwa hawa watafikishwa mahakamani mara uchunguzi wa polisi kwa kushirikiana na maofisa wa shirika utakapokamilika,”alisema.

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya Mhandisi Amosi Maganga, amesema mafanikio ya kukamatwa kwa watuhumia hao yametokana na ushirikiano unaondelea baina ya shirika hilo na wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa za watu ambao wamekuwa wakilihujumu shirika kwa kujihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta pamoja na umeme.

Amesema, shirika limekuwa likiingia hasara kubwa katika upotevu wa mafuta hayo ya Transfoma ambapo ndi chanzo kikubwa cha kusababisha kuungua kwa transfoma hizo, hali inayochangia baadhi ya wanachi kushindwa kupata huduma hiyo ya umeme.

“Ukiangalia katika kipindi cha miezi sita shirika limepata hasara ya shilingi bilioni moja, hivyo ni vema wananchi wakaendelea kutoa ushirikiano ili watu hawa wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria,”alisema.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa na kuwa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahusika atapewa zawadi nono.

Mei 20 mwaka huu Tanesco Mkoa wa Mbeya, lilimkamata Mwantika likimtuhumu kujiunganishia umeme kinyemela na majirani zake na tayari amefikishwa mahakamani.


Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top