Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt .Abdallah Kigoda
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo  TCCIA Mkoa wa Mbeya Dkt Lwitiko Mwakalukwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Mbeya Intarnational Trade Fair.

Na Emanuel Madafa,Mbeya
WAZIRI wa Viwanda na  Biashara Dkt. Abdallah Kigoda anatalajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonesho ya kibiashara (Mbeya  International Trade Fair )yaliyoandaliwa na chama cha wafanyabiashara Kilimo na Viwanda( TCCIA ) Mkoa wa  Mbeya.

Maonesho hayo yatafanyika katika ukumbi wa mikutano Mkapa kuanzia Octoba 23 hadi 29  na kuhudhuriwa na  washiriki washiriki zaidi ya 200 kutoka katika nchi za Kenya Malawi Zambia na Mexico .

Nchi nyingine ni pamoja na Cuba, Syria , Japan  na India pamoja  na makampuni  ya nje yaliyowekeza  Mkoani Mbeya.

Akizungumza jijini Mbeya Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mbeya Daktari Lwitiko Mwakalukwa amesema lengo kuu la maonesho hayo ni kuonesha fursa zilizopo kanda  za juu Kusini hususani Mkoani hapa.

Amesema lengo jingine ni kuwezesha kufanyika kwa biashara za mipakani bila kuwepo kwa vikwazo sanjali na kutambua bidhaa zinazozalishwa katika nchi zilizopo jirani na Tanzania hususani ,Malawi, Zambia na Congo  pamoja na msumbiji .

Aidha amebainisha kuwa kufanyika kwa maonesho hayo kutatoa  fursa pekee kwa wajasilimali wa mkoa huo kuona ubora wa bidhaa  toka nje ya nchi  pamoja na kubadilishana uzowefu  katika kufanya biashara  na kupata masoko.

Kauli mbiu ya maonesho hao ni kutangaza na kukuza biashara  ya mipakani na mkoa wa mbeya kama  fursa mpaya ya uwekezaji.
Mwisho.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top