Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi


Na mwandishi wetu
MTOTO wa miaka saba(7) Ireene Marco, amepoteza maisha baada ya kupigwa  na baba yake kwa kosa la kuzurula ovyo.

Marehemu Ireen ni mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi ya Migombani katika mji mdogo wa Tunduma Wilayani Momba na kwamba alifariki wakati akipatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amesema tukio hilo limetokea juzi asubuhi katika eneo la Sogea Kata ya Tunduma.

Amesema, marehemu alipigwa kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza fahamu  na baba yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Marco Mbembela(30) mkazi wa Sogea.

Aidha, Msangi amesema kuwa  mtuhumiwa amekamatwa na kwamba  upelelezi  umekamilika hivyo atafikishwa mahakamani  kesho(leo).

Hata hivyo Kamanda Msangi, amewataka wazazi na walezi kutumia busara katika kuwaelekeza watoto wakikosea si kujichukulia sheria mkononi.
 mwishoo

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top