Meneja Kituo Cha Uwekezaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Daud Liganda akitoa maelezo juu yakukua kwa sekta ya uwekezaji katika Ukanda huo. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
HALI ya uwekezaji kwa Mikoa ya
Nyanda za juu Kusini, imetajwa kuridhisha kulingana na sekta mbalimbali ambazo
zinampa fursa mwekezaji kuamua kuwekeza eneo analo lihitaji
ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kuanzia mwaka 2008.
Hayo yamesemwa na Meneja wa
uwekezaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Daud Liganda, ambapo amedai kuwa idadi
ya miradi iliyosajiliwa na kituo hicho imeendelea kukua hasa katika sekta
ya kilimo na ufugaji.
Amesema licha ya ukuaji huo kwa kasi
lakini bado umekuwa hauendani na hali
halisi ya maeneo husika hasa kutokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya
kiuwekezaji ambayo kama yakitumiwa vyema ukuaji huo utazidi kukuwa kwa kiwango
kizuri zaidi ukilinganishwa na kipindi hicho cha miaka mitano iliyopita. .
Amesema katika ukanda huo kuna
ardhi ya kutosha na yenye rutuba nzuri pamoja na mvua za mara kwa
mara zenye uwezo mkubwa wa kustawisha mazao ya aina yote.
Aidha Meneja huyo amedai kuwa licha
ya sekta za kilimo na ufugaji kukuwa kwa kiwango kizuri pia Sekta ya Utalii
nayo imezidi kupanda hasa katika ongezeko la ujenzi wa hoteli za
kisasa zenye hadhi ya kimataifa.
Pamoja na ongezeko hilo pia
meneja huyo amewataka wafanyabiashara wa ukanda huo hasa kwa mkoa wa
mbeya kuhakikisha wanaendana na uwepo wa uwanja wa kimataifa wa Songwe ambao
umetoa fursa kubwa hasa katika sekta ya utalii.
Amesema kuwepo kwa uwanja huo
kutafanya kuongeza idadi ya wageni ambao watahitaji kupata sehemu bora kwa
ajili maradhi hivyo nivema wafanyabiashara hao wakachangamkia fursa
hiyo.
Amesema bado kituo hicho kinatoa rai
kwa wadau mbalimbali katika ukanda huo kuendelea kuchangamkia fursa hizo ili
kuweze kuendana na hali halisi ya ukuaji katika nyanja ya kiuwekezaji katika
ukanda huo..
Mwisho
Post a Comment