Mwenyekiti chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Mbeya (MREFA)Ndugu Elias Mwanjala. |
Na mwandishi wetu,mbeya
CHAMA
cha Soka mkoani Mbeya, MREFA, kimekanusha viongozi wake kuhusika na tuhuma za
uingizaji wa tiketi bandia kwenye michezo ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara
katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mkoani humo.
Hatua
hiyo ya MREFA, inafuatia tuhuma zilizotolewa na uongozi wa timu ya Mbeya City
kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanahujumu mapato uwanjani hapo kwa
kushiriki vitendo vya uingizaji wa tiketi bandia kwenye mauzo wakati wa michezo
ya timu hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa MREFA, Elias Mwanjala, amesema hakuna
kiongozi wa chama hicho anayejihusisha na vitendo hivyo bali yaliyopo ni madai
yasiyokuwa na ukweli kutoka kwa viongozi wa Mbeya City.
Mwanjala,
amesema licha ya viongozi wa Mbeya City kumtajia majina ya baadhi ya viongozi
wa MREFA wakidai ndiyo wahusika wa vitendo hivyo lakiini hakuna ushahidi wowote
kuwa wanahusika na tuhuma hizo.
Uongozi
wa Mbeya city kupitia kwa Katibu wake, Emmanule Kimbe, ulidai kuwa baadhi ya
viongozi wa MREFA wanaongoza vitendo vya uingizaji wa tiketi bandia uwanjani
hapo.
Kimbe,
alidai licha ya kuwakataa viongozi hao kuwa ni chanzo cha kuhujumu mapato kwenye
uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine lakini bado wanaendelea kuratibu masuala ya
tiketi uwanjani hapo hali ambayo inawakatisha tamaa kuwa chama hicho
kinawakumbatia watu wasio waaminifu katika mapato.
Malumbano
baina ya pande hizo yameshika kasi zaidi hasa baada ya Mbeya City kudai kuwa
tiketi bandia zaidi ya 500 ziliingizwa kwenye mauzo ya mchezo baina yake na
Simba Februari 15 mwaka huu uwanjani hapo ingawa TFF kupitia kwa Afisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, imeshafafanua kuwa tiketi hizo
si bandia bali zilisahauliwa wakati wa zoezi la kupiga mihuri vitabu vya tiketi
za mchezo huo.
Mbeya
City inaendelea kupinga taarifa hizo kwa maelezo kuwa haiwezekani tiketi zote
500 zilizotokana na vitabu vitano kusahaulika na wapiga mihuri wote
walioshiriki zoezi hilo kutoka timu zote za Simba na Mbeya City.
Mwisho
Picha na Maktaba
Post a Comment