Na Mwandishi wetu,Mbeya
ZAIDI ya Wachimbaji wadogowadogo 2000 wa uchimbaji wa madini ya kokoto
,mawe na mchanga pamoja na madereva wa
maroli yanayojishughulisha na ubebaji wa malighafi hizo wameandamana hadi kwenye ofisi za halmashauri ya Jiji la
Mbeya, kupinga uamuzi wa Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ushuru wa maroli
ya mchanga.
Wakizungumza
na nje ya ofisi za jiji wamesema kitendo cha serikali kuingiza utaratibu wa kuyatoza ushuru magari
ya ubebaji kiasi cha shilingi 2500 kwa kila tripu ni ukandamizaji.
Wamesema,
wao hawapingani na uamuzi wa serikali wa
kuanzisha udhibiti wa uzalishaji na biashara ya madini ya ujenzi na
viwanda tatizo ni kushindwa kuweka wazi mfumo wa tozo la kodi kwa upande wa
magari yanayojihusisha na ubebaji wa
madini hayo.
Aidha,
wafanyabiashara hao waliiomba serikali kuangalia utaratibu wa kuwapunguzia
gharama ya lesseni ya uzalishaji biashara ya madini kwani kiasi cha fedha kilichoainishwa ni kikubwa
ukilinganisha na hali halisi ya kipato cha mtanzania kwa siku.
Akijibu
malalamiko hayo Afisa mfawidhi wa ofisi ndogo ya wakala wa madini Mbeya, Jumanne
Mohamed, amesema kwa mujibu wa sheria zao mlipaji wa mrabaha ni mchimbaji na si dereva .
“Wizara
kupitia waraka huu imeweka wazi kwamba mlipaji wa mrabaha ni mchimbaji
na kwamba hairuhusiwi kuchimba bila ya kuwa na lesseni hivyo hii shilingi 2500
inalipwa na mchimbaji,”alisema.
Amesema,
mchimbaji anapolipia kiasi cha shilingi 2500 hukabidhiwa hati ya malipo ambayo hutolewa bure na kwamba hati hiyo anatakiwa kumkabidhi dereva ili asikamatwe na
kutozwa faini kutoka kwa watendaji wa madini.
Amesema
suala la ulipaji wa mrahaba huo uko palepale kwa mujibu wa sheria hivyo nivyema
taratibu zikafatwa katika kukamilisha zoezi hilo.
Hata hivyo
amewatoa hofu madereva wa malori hayo kuwa kimsingi wao hawahusiki na ulipaji
wa mrahaba huo badala yake mchimbaji ndio anayeusika na mrahaba huo.
Mwisho.
|
Post a Comment