Meya wa jiji la mbeya Ndugu Atanas Kapunga akizungumzia juu ya kuanza kwa ujenzi katika eneo la Soko la Machinjioni Nonde jijini humo |
Hili ndio eneo la soko la machinjioni Kata ya Itigi jijini mbeya ambalo litahamishwa na kujengwa kituo cha afya. |
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya
inatarajia kutumia shilingi milioni 36 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa
kituo cha afya katika kata ya Itiji iliyopo Jijini Mbeya.
Akizungumzia kuanza kwa ujezni huo Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas
Kapunga, amesema Zahanati hiyo inajengwa katika eneo lililokuwa soko la
wakulima.
Asema, kutokana na kujengwa
kwa kituo hicho cha afya wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakiendesha
shughuli zao kwenye soko hilo wataondolewa na kutafutiwa eneo lingine.
Amesema, ujenzi wa Zahanati
hiyo unatarajia kukamilikia katika kipindi cha miezi mitatu hivyo
ifikapo mwezi Juni mwaka huu kituo hicho kitakuwa kimekamilika na
kuanza kufanya kazi.
Aidha, Kapunga amesema endapo
serikali haitafikisha fedha hizo kwa wakati basi yeye atawaomba tena
marafiki zake kumchangia na fedha zitakazo patikana zitaendeleza ujenzi
huo.
Hata hivyo, amewaomba wakulima hao
ambao walikuwa wakilitumiaeneo hilo kuuza mazao yao kutokuwa na wasiwasi kwani
halmashauri inatarajia kujenga soko kwenye Kata hiyo huku eneo la muda
likiandaliwa.
Amesema pamoja na mipango hiyo pia
watahakikisha wanaboresha mazingira ya soko hilo kwa kuweka vyoo ambayo
viatripiwa kwa gharama ndogo ili kulinda afya za watu hao pamoja na walaji.
Mwisho
Post a Comment