Mmoja wa wahanga akiwa nje ya nyumba yake Ndugu Gaby Abson mwenye familia ya watoto wanne akiwa hajui nini cha kufanya. |
Diwani Kata ya Itezi Ndugu Franky Mahemba |
Mwenyekiti Mtaa wa Itezi Mwasote Magharibi Ndugu Peter Mwasote |
UMLA ya nyumba tisa
zimeezuliwa paa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali
kunyesha Jijini Mbeya.
Mvua hiyo ilianza kunyesha Machi 15
mwaka huu majira ya saa kumi za jioni
hivyo kuleta mahafa hayo katika kijiji cha Mwasote kilichopo Kata ya
Uyole ndani ya Jiji la Mbeya.
Akizungumzia hali hiyo Mwenyekiti wa
Mtaa wa Mwasote Magharibi Ndugu Peter
Lingo amebainisha kuwa mvua hiyo imeezua
nyumba 9 na kusababisha baadhi ya kaya kukosa mahali pa kuishi.
Aidha, amesema, tayari
ameshamtahalifu Diwani wa Kata hiyo na kwamba serikali ya kijiji
imetembelea eneo husika na kujionea hali halisi ya wananchi
waliokumbwa na mahafa hayo wakiwa wamejihifadhi kwa ndugu na jamaa zao.
Amesema, tathimini ya hasara na
idadi halisi ya kaya zilizozulika na mvua hiyo bado hazijapatikana hadi pale
ungoiz toka Halmashauri ya jiji utakapo fika katika eneo hilo .
Hata hivyo amezitaka mamlaka husika
kuliangalia suala hilo kwa uharaka zaidi ili kuokoa zaidi maafa mengine hasa
kutokana na mvua hizo kuendelea kunyesha.
Mwisho.
Post a Comment