Watoto hao Elebia Bonifasi( 13) na Iren Bonifas( 12) wakiwa katika ofisi za Ofisa Mtendaji Kata ya Nzovwe jiji Mbeya kwa lengo la kutaka msaada zaidi waweze kulejea shule. |
Mtoto Elebia akionyesha mguu wake ambao umekuwa ukimpa shida kwa muda mrefu sasa ambao umekuwa ukijaa na kuwa mkuba mara umri wake unavyo zidi kuongezeka. |
Nyumbani kwa dada yeo ambapo kwa sasa wanaishi watoto hao eneo la Nzovwe jijini mbeya. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Vitendo vya kikatiri na
unyanyasaji kwa watoto bado vimeendelea kulikumba jiji la Mbeya ambapo katika hali
isiyokuwa ya kwaida wanafunzi wawili wa kike Mmoja wao akiwa ni
mlemavu wa mguu wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Jitegemee
Nzovwe Iliyopo Jijini Mbeya wameshindwa kuendelea na elimu hiyo baada ya
kuondokewa na wazazi wa pande zote mbili huku mlezi aliyechukua jukumu la
kuwatunza kudaiwa kuwakatisha masomo na kuwatumikisha
mashambani.
Wanafunzi hao ambao ni
Elebia Bonifance (13) na Iren Bonifance (12) wote ni wanafunzi wa darasa la
saba katika shule ya msingi ya Jitegemee wameshindwa kuendelea na masomo hayo
katika kipindi cha miezi mitatu baada ya wazazi wao kufariki.
Akizungumza na Jamiimoja wakiwa katika ofisi za Mtendaji Kata ya Nzovwe
watoto hao ambao mmoja kati yao Elebia Bonifance kupatwa na ugonjwa wa
mguu wake mmoja kukua kila mwezi licha ya kukatwa vidole vyake viwili
ambavyo vinadaiwa kugundulika kuwa na tatizo la tezi.
Akisimulia maswaiba ya
ugonjwa wa mguu huo, mtoto Elebia amesema kuwa alizaliwa akiwa amevimba
vidole hivyo viwili vya mguu wa kushoto na kila alipokuwa anakua na vyenyewe
viliendelea kukua na kuzidi umri wake ndipo mama yake alipoamua kumpeleka
hospitali na kukatwa akiwa na umri wa miaka tisa.
Amesema, baada ya
kukatwa vidole hivyo kidonda kilikauka lakini cha ajabu ni kwamba mguu huo
unaendelea kuvimba hasa nyakati za mchana kutokana na kupigwa na jua lakini
maumivu hayasikii.
Amesema, maisha
wanayoishi yeye na mdogo wake ni ya tabu sana kwani mara baada ya mama
yao kufariki walichukuliwa na baba yao mkubwa waliomtaja kwa jina la James
ambaye ameoa wanawake wawili hivyo wao kuishi na mama yao mkubwa ambaye amekuwa
akiwatumikisha kazi mashambani.
Amefafanua kuwa wakati wanachukuliwaa waliwaeleza kuwa watawapeleka shule lakini mpaka sasa wanashangaa
kila siku zinavyozidi shuleni hawaoni dalili zozote huku mama mkubwa wao akichukua jukumu la kuwapeleka shambani kulima tena bila ya kula hali ambayo
iliwarazimu kutoroka.
Amesema, akiwa
shambani mguu wake ulikuwa ukimuuma sana kutokana na jua hivyo mdogo wake
kumuonea huruma na kumtaka watoroke na kurudi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi
marehemu mama yao ambayo alipewa na rafiki yake kujihifadhi.
.
Aidha, juhudi za kumtafuta
Dada yao zilianza ambapo ilifanikiwa
kuzungumza na dada wa watoto hao Subi Bonifance mkazi wa Nzovwe
ambaye alikiri kupata shida kwa wadogo zake na yeye kushindwa kuwasaidia
kutokana na kujifungua mtoto mchanga wa wiki mbili.
Kwa sasa yeye binafsi
hana uwezo wowote wa kuwalea wadogo zake
hao kwani mumewe ambaye ndiye anayetoa feza kwa ajili ya maradhi na chakula
amekuwa akipingana na suala la kukaa na watoto hao hivyo anahitaji msaada wa
haraka ili aweze kuwahudumia wadogo zake hao.
.
Kwa upande wake Afisa
ustawi wa jamii Habiba Ibrahim,alisema kuwa suala la mtoto huyo wanalifahamu na
kwamba wakati wakiwa katika mahojiano na mama mzazi wa mtoto huyo na
kuanga uwezekano wa kumsaidia ndipo mama huyo alipofariki na watoto hao
kutokomea wasipojulikana.
mwisho
Post a Comment