Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jengo ambalo litatumika kwa ajili ya kuwekea mitambo wa kisasa wa   kukobolea mpunga katika kijiji cha Kipusya Wilayani Kyela Mkoani Mbeya likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo

Mkuu wa mkoa wa mbeya Abbas Kandoro akizungumza na wananchi wa kijiji hicho ambao ndio wanufaika wakubwa wa mradi huo.

Wananchi na baadhi ya viongozi wa Wilaya hiyo ya Kyela wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa

Mkuu wa Wilya hiyo ya Kyela Ndugu Magreth Simalenga akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa Ndugu Abbas Kandoro juu ya utekelezaji wa mradi .





Na EmanuelMadafa,Mbeya.


SERIKALI Mkaoni Mbeya, imetumia shilingi milioni 200 kwa  ajili ya ujenzi wa jengo la mashine  ya kisasa ya kukoboa mpunga pamoja na uvutaji wa umeme wa njia kuu yenye transfoma Wilayani Kyela.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abasi Kandoro, alisema  serikali imeanzisha mradi huo, lengo likiwa ni kuongeza kipato kwa wafanyabiashara kwa kuwaongezea thamani zao la mpunga.



Amesema, mashine hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo mkubwa wa kukoboa, kupanga madaraja na kufungasha  zao hilo la biashara kwa wakulima wa kijiji cha Kikusya Wilayani Kyela.



Aidha, Mkuu  huyo amewataka wafanyabiashara  hao kuhakikisa wanatumia mashine hiyo vizuri kwani itasaidia kuongeza thamani ya zao hilo la mpunga ambalo kwa sasa limeanza kupoteza umaharufu wake kwa kuchakachuliwa na wachuuzi kutoka mikoa mingine.





Amesema,  serikali  imejipanga katika kuhakikisha inamkomboa mkulima  kwa kuhakikisha inawajengea mazingira mazuri ili waweze kufikia malengo yao.



Kufuatia hali hiyo ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha unakaa na wakulima na wafanyabiashara wa zao  hilo kubuni jina  jipya la mchele wa kyela  ambao utaweza kuendana na soko la kiushindani la kimataifa tofauti na sasa.



Wachuuzi wa  mpunga kutoka mikoa mbalimabali ya nchi wameuchakachua mchele wa Kyela hivyo kuharibu jina halisi hali iliyochangia kwa mchele huu kukosa wateja ni vema sasa wakulima na uongozi wa halmashauri ukakaa meza moja na kuangalia uwezekano wa kubadilisha jina,”amesema.


Amesema, mchele wa kyela umepoteza umaarufu wake kutokana na kuibuka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa wakitumia jina hilo vibaya kwa kuchanganya na aina nyingine ya mchele hivyo kushusha uthamani wake .



Mwishoo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top