Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akitoa maagizo kwa uongozi wa kijiji cha Kingili pamoja na viongozi wengine wa Wilaya juu uhamasishaji wakulima kutumia njia bora za kilimo cha mpunga . |
Kandoro akizungumza na wananchi wa vijiji vya jirani na mradi huo wa skimu ya umwagiliaji namna ya kutumia fursa hiyo kujinufaisha badala ya kuacha kilimo na kukimbilia mjini ambako hakuna ajira. |
Diwani wa Kata ya Ipinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Kyela Daktari Hanta Mwindaji akifafanua jambo kuhusiana na mradi huo. |
Wananchi nao hawakuwa mbali kuishukuru serikali juu ya kuwapelekea mradi huo. |
Na Mwandishi wetu,
Mkuu wa mkoa Mbeya bwana Abasi
Kandoro ameuagiza uongozi wa kijiji cha Kingili Kata ya Ipinda Wilayani Kyela
Mkoani Mbeya kuhakikisha wanahamasisha wakulima juu ya kuachana na kilimo cha
kizamani Cha mpunga na kujikita katika ulimaji wa kisasa kwa kutumia njia
bora za kitaalam.
Amesema kwa muda mrefu sasa wakulima wamekuwa wakijishughulisha na shughuli za Kilimo bila kuwa na mafanikio yoyote hasa kutokana na kuendeleza kilimo cha mazoea.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo Wilayani Kyela Mara baada ya kutembelea mradi wa Kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Kingili kata ya Ipinda mradi ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni28 zilizotolewa na serikali kwa lengo la kuinua kilimo cha umwagiliaji wilayani humo.
Kandoro amesema nivema sasa wakulima wakaachana na kilimo cha mazoea bila kufuata taratibu za kitaamu Hali ambayo ime fanya wakulima wengi kuendelea kuwa masikini na kushindwa kufikia malengo Yao.
Amesema Kilimo cha kutupa kwa mkono ni Kilimo cha kizamani sana ambacho hakiwezi kuwaondoa wakulima hao katika umasikini hivyo umefika wakati kwa viongozi pamoja na wataalamu kushirikiana kwa ukaribu kwa lengo la kumkomboa mkulima huyo.
Amesema katika kuhakikisha mkulima ananufaika na Kilimo chake serikali imeamua kuanzisha mradi wa kukoboa mpunga katika kijiji cha kapusyi wilayani Kyela Mkoani humo ambao umegharimu kiasi cha shilingi milion 200 ambapo lengo lake ni kumfanya mkulima aendelee kunufaika na zao hilo la mpunga.

Amesema ili mtambo huo uweze kufanya kazi zake vizuri zilizokusudiwa lazima wakulima wa zao la mpunga katika mabonde yote Nane ya mpunga katika Wilaya hiyo ya kyela waakachana na Kilimo hicho cha mazoea badala yake waingize utaalam.
MWISHO
Post a Comment