Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakisubiri viongozi wa serikali kata ya Itezi jijini mbeya kwa lengo la kusuhulisha mgogoro uliopo ndani ya kanisa hilo. |
Diwani wa Kata ya Itezi jijini Mbeya Ndugu Frank Mayemba akizungumza na waumini na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo kujua kini cha mgogoro huo |
Mmoja wa waumni wa kanisa hilo ambaye ndiye anayedaiwa kuwa mmiliki wa eneo hilo la mgogoro |
Na Mwandishi wetu.
WANANCHI wa Mkoa wa Mbeya, wameiomba
serikali kuangalia utaratibu wa kusitisha usajili wa makanisa ili
kupunguza migogoro katika jamii.
Ombi hilo limekuja kufuatia
kuibuka kwa mgogoro ndani ya kanisa la House of Prayer Shield of Faith
Christian Fellowship la Jijini Mbeya baada ya muumini kuamua kunyang’anya
eneo lake la ardhi alilolitoa kwa ajili ya kujenga nyumba ya muda ya ibada.
Mgogoro huo, umesababisa
uongozi wa kanisa kulifikisha suala hilo polisi huku baadhi ya
waumini wakimtaka muumini huyo kuwarudishia kiasi cha fedha cha shilingi
milioni 1,000,000/= ambacho walijitolea kufyatua matofali.
Akizungumza jijini Mbeya , Mzee
Amani Mwafongo (75) Mkazi wa Kata ya Itezi Jijini Mbeya,alisema kuwa
tatizo lililopo ni serikali kutoa uhuru mkubwa wa watu kuanzisha makanisa yao.
Mzee Amani, ameshawahi kushika
natafasi ya Mwenyekiti Taifa wa Kanisa hilo na kufukuzwa baada ya
kutofautiana na matakwa ya kiongozi wao mkuu, alisema makanisa
mengi ya sasa yamekuwa yakitanguliza maslahi binafsi mbele badala
yakusimamia huduma ya kiroho.
“Makanisa mengi yasiyozingatia
maadili ya kiroho yamekuwa yakianzishwa ovyo, hii inatokana na serikali
kutoa uhuru uliopitiliza,”alisema.
Amesema, athari ya kutodhibitiwa kwa
makanisa hayo ni kukithiri kwa migogoro isiyokuwa na maana na yote hiyo
husababishwa na tamaa na maslahi binafsi waliyotanguliza wamiliki wa makanisa
hayo.
“Endapo serikali itaendelea kuyalea
makanisa haya yanayojiita ni makanisa ya kutoa huduma ya kiroho kuendelea
kuibuka yanaweza kuleta maafa makubwa,”alisema.
Aidha,amesema wamiliki hao wamekuwa
wakiaanzisha makanisa na kuwatumia wachungaji pasipo walipa mishahara
yao hivyo mchungaji anapoamua kutafuta njia nyingine ya kujipatia kipato
basi uongozi uingilia kati na kumfukuza.
mwisho
Post a Comment