Mama Mjane mwenye watoto watano Mkazi wa Inyala Kata ya Iyunga Bi.Sharfa Adam akiwa katika Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Inyala kwa lengo kuonana na uongozi. |
Nyumba ya Mama huyo aliyo achiwa na marehemu Mme wake ambayo kwa sasa anaishi hapo. |
Licha wanawake Duniani Kote wakiwa katika maandalizi ya kusherekea siku yao ambayo inatarajiwa kuadhimishwa Machi 8 mwaka huu bado idadi kubwa ya wanawake mkoani mbeya wameendelea kuishi katika mazingira magumu mara baada ya waume zao kufariki dunia kutokana na sababu mbalimbali na kuwa acha wakiwa wajane.
Katika
tukio la kusikitisha Mkazi wa Inyala Kata ya Iyunga jijini Mbeya
Bi.Sharifa Adam( 31) ambaye ni mama mjane mwenye watoto watano amejikuta
katika hali ngumu ya kimaisha kufuatia mume wake kufariki dunia
Februali 27 mwaka huu .
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa mama huyo amedai kuwa amekuwa akiishi katika
mazingira magumu mara baada ya mume wake kufariki duni na kumuachia
mzigo mkubwa wa watoto watano huku yeye akiwa hana shughuli yoyote inayo muingiizia kipato.
Amesema
mume wake alikuwa akijishughulisha na kazi ya Bodaboda katika kituo cha
Iyunga ambapo katika hali ya kusikitisha mumewe huyo aliuliwa na kundi
la watu mara baada ya kumkodisha.
Amesema
mara baada ya kupokea taarifa za kuuwawa kwa mumewe alichukua jukumu la
kutoa taarifa katika kituo cha polisi Iyunga na kwa ndugu wa marehemu
ambapo ulianza msako kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na bodaboda
wenzake ambapo walifanikiwa kuukuta mwili wa muwe wake ukiwa umetelekezwa katika kijiji kimoja wilayani Mbozi.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mama huyo amedai kuwa mara baada ya jeshi la
polisi kufanikiwa kuupata mwiii huo baadae pia pikipiki ya mume wake na
watuhumiwa wote walitiwa mbaroni ambao kwa sasa kesi hiyo ipo kituo cha
polisi kwa ajili ya upelelezi.
Mama
huyo amesema wakati mume wake anafariki alimuachia watoto watano ambao
kati yao watatu walikuwa wakisoma shule ya msingi Ikuti darasa la kwanza
na la pili huku wawili wakiwa wachanga ambao ni mapacha hivyo maisha
yake kwa sasa ni magumu sana na anahitaji msaada wa haraka vinginevyo
atawapoteza watoto wake kutokana na tatizo la njaa.
Hata hivyo amedai kuwa
marehemu mume wake alimuachia nyumba yenye vyumba viwili ambayo bado
hijakamilika hivyo kumfanya aendelee kuishi ndani y nyumba hiyo huku
ikiwa haina madirisha na watato wake watano.
Kufuatia
hali amewaomba wasamalia wema kujitokeza na kumsaidia mama huyo ambapo
pia watoto wake waweze kwenda shule pamoja na mapacha hao kupata lishe
bora.
Hata
hivyo amelitaka Dawati la jinsia la wanawake na watoto mkoani humo
kuhakikisha wanamsaidia kwa haraka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo
hatimaye iyende mahakamani na kutolewa kwa hukumu ili aweze kupta haki
yake.
Bi Sharfa akiwa na baadhi ya watoto wake ambao ni mapacha nje ya nyumba yake ambapo watoto wake wengine wanaishi kwa shemeji yake. |
Mwenyeki wa serikali ya Mtaa wa Inyala Bw.Nelson Mahena akitoa maelekezo kwa mama majane huyo mara baada ya kufika ofisini kwakwe. |
Mama mjane akiwa na watoto wake mapacha ambapo alionyesha kubugujikwa na machozi kutokana na majonzi ya kufiwa na muwewe pamoja na mzigo alio nao |
Picha na Jamiimoja.
Post a Comment