wanafanzi wa shule ya sekondari ya Matema Beach wakiimba wimbo wao wa shule. |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo . |
Mwanafunzi akipata maji safi mara baada kupata na kiu kikali. |
Moja ya jengo jipya linalojengwa shuleni hapo wa msaada wa benki ya Dunia ambalo ni moja ya majengo mapya yanayojengwa shuleni hapo . |
PICHA NA JAMIIMOJA.
Na Mwandishi wetu,Kyela
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ameonyesha kusikitishwa na ufaulu mbovu wa wanafunzi wa kidato cha Nne mwaka 2013 katika shule ya sekondali ya Serikali ya Matema Beach Iliyopo Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.
Hatua hiyo inatokana na shule hiyo kushindwa kufanya vyema katika matokeo yake ya kidato cha Nne kwa mwaka 2013 licha ya shule hiyo kuwa na miundombinu bora kuliko shule zote za Wilaya hiyo .
Akizungumza na Walimu na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutembelea shuleni hapo kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo shuleni hapo Kandoro amedai kuwa inasikitisha kuona shule hiyo inakuwa na miundombinu bora huku ikishindwa kufanya vyema kwenye matokeo.
Amesema yeye anaamini kuwa suala la uwepo wa miundo mbinu bora mashuleni kumekuwa kukichngia kwa asilimia kubwa kwa wanafunzi kufanya vyema kimasomo.
Amesema haiwezekani katika matokeo ya kidato cha Nne mwaka 2013 pasiwepo na hata Daraja la kwanza la ufaulu huku idadi ya waliofeli ikiwa kubwa .
kufutia hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wanafunzi hao kuachana na vitendo viovu vya na kuzingatia masomo pamoja na kufuata misingi na taraibu za shuleni hapo.
Amesema alicho baini kutokana ufaulu huo mbovu ni nidhamu mbovu uliopo miungoni mwa wanafunzi hao hivyo ametoa onyeo kali kwa mwananfuzni yoyote atakye kiuka misngi ya shule hiyo kuwa atafukuzwa shule.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amesema kumekuwepo na tabia ya wanafunzi kufanya vurugu mashuleni na kutegemea ofisi yake kuwa itawaonea huruma na kuwarudisha shuleni hivyo amewataka wanafunzi hao kutambua kuwa endapo mwanafunzi atabainika kufanya utomvu wa nidhamu nilazima akafukuzwa shule bila ya ofisi yake kuingilia kati.
Katika ufaulu wa matokeo ya kidato cha Nne mwaka 2013 jumla ya wanafunzi 121 walifanya mtrihani huo huko ufaulu wa ukiwa mbaya ambapo katika Daraja la 1 hakuna na Daraja la 11 zikiwa 4 na Daraja la 111 zikiwa 10 na 1v zikiwa 49 na 51 zikiwa 0.
Mwishoo.
Post a Comment