Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi. |
Na Mwandishi wetu,
MAHABUSU aliyefahamika kwa jina
la Nasson Paul (70) mkazi wa Ruiwa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya
amejinyonga na kupoteza maisha akiwa ndani ya mahabusu.
Akielezea tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea machi 18 mwaka huu majira ya saa 04:50 alifajili asubuhi katika mahabusu ya polisi iliyopo kituo cha Kati cha Mbeya mjini.
Amesema, marehemu huyo alipoteza maisha muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kupatiwa matibabu..
Msangi, akifafanua kutokea kwa tukio hilo, amesema marehemu huyo akiwa ndani ya chumba chake cha mahabusu inadaiwa alifanya jaribio la kujinyonga kwa kutumia shati lake.
Amesema, akiwa katika harakati hizo za kujiua baadhi ya askari wa zamu aliingia ndani ya chumba hicho ikiwa ni moja ya utaratibu wao wa kukagua na kushuhudia mwili wa mzee huyo ukiwa chini huku akipumua kwa shida.
Amesema, askari hao walimchukua marehemu akiwa katika hali mbaya kwani alikuwa haongei na kumkimbiza hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.
Hata hivyo, Kamanda huyo, amesema kuwa marehemu alikuwa akikabiliwa na kosa la mauaji na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya.

mwisho.
Post a Comment