Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya Uwsa Bi.Neema Stanton akizungumzia juu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji ambapo mwaka huu kilele chake ni Machi 22. |
Moja ya Ziara zilizofanywa na Bodi ya Maji hivi karibuni katika kutembelea vyanzo vya maji katika eneo la Iziwa jijini humo . |
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (Uwsa) imezipongeza kamati za Maji kwa kuweza kuzuia tatizo la uharibifu wa vyanzo vya maji pamoja na uharibifu wa mazingira jijini humo.
Akizungumza jijini Mbeya Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya Bi.Neema Stanton amesema katika kuadhimisha kilele cha wiki ya maji ambayo inatarajiwa kufanyika machi 22 mwaka huu mamlaka hiyo imeridhishwa na namna kamati za maji zinavyo fanya kazi katika kuzuia tatizo la uharibifu wa vyanzo vya maji unaofanywa na baadhi ya wananchi wasio kuwa waaminifu jijini humo.
Amesema kwa kipindi kirefu mamlaka hiyo imekuwa ikipata hasara kubwa kwa kushindwa kuzarisha maji ya kutosha kutokana na vyanzo vya maji kuharibiwa na baadhi wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya vyanzo hivyo vya maji kwa kuendesha shughuli zao za kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji.
Amesema mara baada ya kuliona hilo Mamlaka hiyo iliamua kuanzisha kamati za maji kwa kushirikisha viongoziwa maeneo husika ambao ni Waheshimiwa Madiwani na wenyeviti wa vijiji pamoja na wananchi kwa ujumla wa maeneo hayo ili kuweza kudhibiti hali hayo.
Amesema hatua ya kuanzishwa kwa kamati hizo kumesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la uharibifu wa vyanzo vya maji pamoja na uharibifu wa mazingira ambapo wananchi wameweza kutoa taarifa za mojakwamoja juu ya watu wanaohusika na uharibifu huo.
Amesema kwa sasa wananchi wamekuwa na uwelewa mkubwa juu ya utunzaji swa vyanzo vya maji licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo kutoka kwa wananchi juu ya uwelewa wa jambo hilo.
Hata hivyo amesema endapo uharibifu unatokea katika maneneo ya karibu na vyanzo vya maji wananchi wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo tofauti na kipindi cha nyuma ambapo jukumu hilo liliachiwa kwa mamlak pekee.
Wakati huo huo Afisa habari huyo amesema katika kuelekea siku ya maji duniani bado kuna wateja wasiokuwa waaminifu ambao wameendelea kuihujumu mamlaka hiyo kwa kutumia maji bila kuripa pamoja na kuharibu miundombinu ya mamlaka.
Kufuatia hali hiyo amewataka watu hao kuacha tabia hiyo badala yake wafuate taratibu za upataji huduma ya maji ili shirika hilo liweze kujiendesha pamoja na kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake.
mwisho. .
Post a Comment