Watuhumiwa kesi ya ujambazi january 3 mwaka huu eneo la kawetere nje kidoko ya jiji lambeya wakiwa mahakamani
NaMwandishi wetu.
Kesi ya uporaji inayo wahusu askari wawili
pamoja na Raia watatu ambayo inaendelea katikaMahakama ya Mkoa wa Mbeya imezidi
kuvuta hisia za wakazi wa jiji la mbeya mara baada ya upande wa mashtaka kuzuia ombi la
wakili wa utetezi Ladislaus Rwekiza kutaka kumuuliza maswali
shahidi wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwa madai ya kwamba
wakili huyo alichelewa kufika na kukuta kesi hiyo inasikilizwa.
Kesi hiyo ambayo inawahusisha
washitakiwa watano aliyekuwa askari polisi PC James, askari wa Jeshi la
Magereza Juma Musa, raia wengine watatu, Mbaruku Hamisi ,Amri Kihenya na
Elinaza Mshana ambao wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa la unyang’anyi
wa kutumia silaha na kwamba tukio hilo walilifanya January 3 mwaka huu katika
eneo la Kawatele Wilayani Mbeya.
Ubishi mkali ulianza pale Wakili wa
utetezi Ladislaus Rwekiza kusimama na kuiomba mahakama hiyo iliyokuwa
ikiendeshwa na Hakimu Mfawidhi, Michael Mteite kumpa nafasi ya kumuuliza
shahidi kutoka upande wa mashitaka Filbert Matoho ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi.
Mara tu ya kuwasilisha ombi
hilo ambalo lilipingwa na Wakili wa serikali Achileus Mulisa, ambaye aliitaka
mahakama hiyo kutokubali ombi hilo kwani wakili Rweikiza hawezi kumuhoji
maswali shahidi wake kwakua alichelewa kufika.
Akitatua ubishi huo, hakimu Mteite aliuambia
upande wa mashitaka kwamba haoni sababu ya kumzuia wakili Rweikiza
kutomuuliza shahidi maswali kwani hakuna sheria inayomzuia hivyo kama yeye
anaifahamu aiwasilishe mezani.
Washitakiwa hao walikamatwa
January 3 mwaka huu majira ya 11:45 jioni kwenye mlima Kawetele barabara ya
Chunya-Mbeya, kwa tuhuma za kuhusika kwenye
tukio la kuwapora wafanyabiashara wawili wenye asili ya kiasia mali
mbalimbali.
Mbali na wakili Rweikiza
mawakili wengine kwa upande wa utetezi ni John Steven na Muya Daniel kesi hiyo
itasikilizwa tena March 18 mwaka huu ambapo upande wa mashitaka utaendelea
kuleta mashahidi wake.
Mwisho.
|
Post a Comment