Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wachezaji wa Timu ya Bodaboda wakishangilia ubingwa wao mara baada ya kuchabanga timu ya Bajaji kwa mikwaju ya Penati 4 :1 katika fainali zilizo chezwa katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu jijini Mbeya( TIAA) Machi 16 mwaka huu.




Raha sanaaaa



mwaliiii

Namwaga radhi huweziiiiiiiiii

Kapteni wa Timu ya Bajaji akionyesha ngao mara baada ya kushika nafasi ya pili na kuambulia ngao hiyo pamoja na pesa kiasi cha shilingi laki 3.

Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Mkoani mbeya Bw.Moses ambao nao warishiriki katika michuano hiyo na kuambulia nafasi ya tatu na kupata  kiasi cha shilingi laki Moja.

Skeleu Skelewwwwu.


Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Mbeya (MREFA)Bw.Seleman Harubu akitoa nasaha zake kwa mabingwa na washiriki katika michuano hiyo iliyoandaliwa na mawakala wa magari ya miguu mitatu Bajaj kupitia kampuni ya TVS ambapo katika nasaha zake amezitaka timu shiriki pamoja na wadau wengine kuhakikisha wanasajili timu  zao ili ziweze kutambulika rasmi kisheria .
Harubu amesema umefika wakati sasa timu zote za mipira ya miguu zilizopo mitaani jijini humo pamoja na maeneo mengine wakaanza mikakati ya kusajili timu hizo ili ziweze kutambulika kisheria hali ambayo itawapa nafasi katika kushiriki katika michuano mikubwa.


Amesema endapo timu hizo hazitafanya hivyo hazitoluhusiwa kushiriki katika michuano yoyote ile itakayo andaliwa na wadau hivyo amevitaka vilabu hivyo kuanza mikakati yao mapema ili wasijekutana na dhoruba hilo.

Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa kusajili  timu kuna faida nyingi sana hasa likwemo la ushiriki katika michuano mkubwa kama vile ligi za wilaya na michuano mingine.

Fainali hizo zililenga kuwaonganisha wananchi pamoja na jeshi la Polisi mkoani humo ambapo bingwa katika michuano hiyo ni timu ya Bodaboda iliyoichabanga Bajaj kwa mikwaju ya penati  mara baada ya kutoka sare kwa goli moja moja ambapo bingwa huyo ameondoka na kitita cha shilingi laki 3 na kombe huku mshindi wa pili akiondoka na kitita cha shilingi laki 2 na laki 1 kwa mshindi wa tatu.

mwishoo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top