Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na EmanuelMadafa,mbeya
Zaidi ya Abiria 15 waliokuwa wasafiri katika bus la Kampuni ya Princes Muro wafika salama jijini Dar Salaam kwa Kampuni ya usafirishaji ya News Force inayofanya safari zake Dare es salaam Tunduma.

Abiria hao walikwama kuondoka jijini humo kwamadai kuwa lilikuwa limeharibika muda mfupi kabla ya kutaka kuondoka kwa mujibu wa ratiba yake ya kila siku.
  
Aidha abiria hao walifikakatika stendi kuu ya mabasi majira ya saa12 na Nusu ambapo mara baada ya kufika kituoni hapo walielezwa kuwa basi lao halita weza kuondoka kutokana na kuwepo kwa hitirafu hiyo.

Kitendo hicho kiliwakwaza abiria hao na kuanza kuomba msaada kwa lengo la kurudishiwa nauli zaa pamoja na kutafutiwa usafiri mwingine.


Mvutano huo uliwaladhimu baadhi ya wananchi waliokuwepo katika kituo hicho cha Mabasi yaendayo mikoani jijini Mbeya kuingilia kati kwa lengo la kuwasaidia abiria hao kupata usafiri.

Aidha juhudi hizo zilizaa matunda ambapo uongozi wa kampuni hiyo ulilazimika kuonana na uongozi wa kampuni ya Newsforce kwa lengo la kuchukua abiria hao ambapo hata hivyo walifanikiwa kuondoka katika majira ya saa2 na nusu asabuhi.

Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa abiria hao ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema kuwa wamefika salama jijini Dar es Salaam bila kupata usumbufui wa aina yoyote.






Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top