Na EmanuelMadafa,Mbeya
Halmashauri
ya Wilaya Mbeya Mkoani Mbeya kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu wameazimia kuweka mikakati ya pamoja katika kuhakikisha
Sekta ya Elimu inakuwa katika Halmashauri hiyo.
Moja ya
mikakati hiyo ni kuboresha mazingira ya walimu pamoja na kuboresha miundombinu
ya Ufundishaji.
Awali
akifungua Mkutano wa Kujadili taarifa mbalimbali za elimu katika Halmashauri
hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Nouman Sigalla amewataka viongozi wa halmashauri hiyo kuacha kufanya kazi kwa
mazoea badala yake wajikite katika kubuni mbinu mpya itakayosaidia kuinua
kiwango cha Elimu wilayani humo.
Amesema katika
kuhakikisha kiwango cha Elimu kinakuwa katika Halmashauri hiyo nivyema kila
kiongozi akawajibika na kutimiza wajibu kwa nafasi yake bila kujali nafasi aliyonayo.
Aidha Mkuu
huyo wa Wilaya amebaisha kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za
kielimu hususani upungufu wa Nyumba za walimu na uchache wa walimu kusiwe
kikwazo cha kushindwa kufaulisha wanafunzi.
Hata hivyo
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka viongozi hao kuwa wakali katika kusimamia suala
hilo vinginevyo Halmashauri hiyo itakuwa nyuma kielimu pamoja na kushindwa
kufikia lengo lake.
Katika hatua
nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Madiwani wa Halmashauri hiyo kuhakikisha
wanahamasisha wazazi katika suala ulipaji wa ada kwa wakati ili kuondoa usubufu kwa walimu.
Amesema
kumeibuka kwa mtindo kwa baadhi ya wazazi kushindwa kulipa ada kwa wakati hali ambayo inawalazimu walimu kuacha
kufundisha na kujikita katika suala la
ufuatiliaji wa ada kwa wanafunzi.
Katika
Matokeo ya Darasa la Saba 2013/14 Halmashauri hiyo imeshika nafasi ya 8 kimkoa huku Secondari ikiwa katika nafasi ya
7.
Mwisho.
Post a Comment