Na EmanuelMadafa,Mbeya
MTOTO wa miaka mitatu Vanesa Patrick, amepoteza maisha baada ya kupigwa
ngumi na baba yake mzazi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amesema tukio hilo
limetokea juzi majira ya saa tano za usiku katika Kijiji cha Isisi Kata ya
Rujewa Wilayani Mbarali.
Amesema, katika tukio hilo Polisi wanamshikilia baba wa mtoto huyo
aliyemtaja kwa jina la Patrick Njojo(23) mkazi wa kijiji cha Isisi.
Aidha, akielezea tukio hilo Kamanda Msangi, amesema inasemekana kuwa baba
huyo alikuwa amelewa baada ya kunywa pombe za kienyeji hivyo
kutenda kosa hilo.
Hata hivyo, amesema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi utakapo
kamilika baba huyo atafikishwa mahakamani.
Mwisho.
Post a Comment