Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Crispin Meela |
Na
EmanuelMadafa, Mbeya.
MWALIMU
Maiko Mwakapala wa Shule ya msingi Mchanganyiko iliyopo Wilayani Rungwe
Mkoani Mbeya, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa
la nne ambaye ni mlemavu wa macho.
Mwalimu huyo
ambaye naye ni mlemavu wa macho inadaiwa kutenda kosa hilo April 25 mwaka
huu siku ya Ijumaa jioni.
Akizungumza
na blog hii kwa sharti la kutoja jina
lake wala picha mwalimu mkuu wa shule hiyo amekiri kuwepo kwa
tukio hilo na kwamba tayari mwalimu Maiko amefikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Amesema,
siku ya Ijumaa jioniApril25 mwaka huu Mwalimu Maiko alikutwa na mwanafunzi huyo
nyumbani kwake akitaka kumwiingilia kimwili hivyo walimkamata na kumfikisha
kituo cha polisi.
Akizungumzia
tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya
ya Rungwe, Chrispin Meela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
tayari mwalimu huyo amekamatwa.
Aidha, Meela
amesema kuwa uchunguzi wa awali aliofanyiwa mwanafunzi huyo umeonyesha kwamba
mtoto huyo alikuwa hajaingiliwa kwa siku hiyo lakini amekutwa na magonjwa ya
zinaa.
Kwa mujibu
wa Meela. amesema mwanafunzi huyo alikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
mwalimu na kwamba taratibu za kumfanyia vipimo Mwalimu Maiko zinafanyika.
Hata hivyo,
Mkuu huyo amesema serikali haitalifumbia macho suala hilo kwani yeye binafsi
ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo yenye mchanganyiko wa wanafunzi wa kawaida na
walemavu atahakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.
Mwisho.
Post a Comment