Kamanda wa Polisi Mkoani mbeya Ahmed Msangi |
EmanuelMadafa,MBEYA
Jeshi
la Polisi Mkoani Mbeya limewahakikishia wananchi wa mkoa kusherekea sikuku ya pasaka kwa amani na
Utulivu.
Aidha, Jeshi hilo linatoa wito kwa Kila Mwananchi kuona
wajibu wa kufuata na kutii sheria
zilizowekwa bila kushurutishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ahmed Msangi amesema katika kuelekea katika
sherehe za sikuku Pasaka jeshi hilo limejipanga vyema katika kuhakikisha
wananchi wa mkoa wa mbeya wanasherekea kwa amani na Utulivu.
Hata Hivyo Kamanda Msangi amewataka wazazi na walezi
mkoani humo kuacha muangalizi/waangalizi
nyumbani wanapotoka kwenda katika Ibada za Mkesha na Sherehe kwa jumla kwa
ajili ya ulinzi na usalama wa mali zao.
Pia amewataka watumiaji wa Vyombo vya Moto kuhakikisha
wanafuata na kuzingatia Sheria na Alama za Usalama Barabarani ili kuepuka ajali
Pamoja na watembea kwa miguu kuwa makini na matumizi ya barabara ikiwa ni
pamoja na kuvuka katika maeneo yenye vivuko [zebra crossing].
Aidha Kamanda wa Polisi anawataka wazazi/walezi kuwa
makini na watoto wadogo kwa kutowaacha wakatembea bila uangalizi wa kutosha.
Pamoja hali hiyo pia Wamiliki wa kumbi za Starehe kuhakikisha
wanazingatia taratibu za uendeshaji wa
Biashara zao ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Mwisho
Post a Comment