Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Matukio na makosa
ya usalama barabarani katika Mkoa wa Mbeya imetajwa kupungua kwa kiwango cha
asilimia 15 katika kipindi cha mwezi Januar hada machi mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya
Ahmed Msangi akizungumza jijini Mbeya amesema kuwa jumla ya makosa na matukio yote
yaliyoripotiwa katika kipindi cha Jan – Machi,
2014 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na
usafirishaji ni 12,250 wakati
kipindi kama hicho Jan-Machi, 2013
yaliripotiwa makosa 14,375 hivyo
kuna pungufu ya makosa 2,125 sawa na asilimia 15.
Amesema Matukio ya ajali
yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Jan –
Machi, 2014 yalikuwa 98 wakati
kipindi cha Jan- Machi, 2013 yalikuwa
156 hivyo kufanya kuwepo kwa na upungufu wa matukio 58 sawa na asilimia 37.
Msangi ameabainisha kuwa Matukio
ya ajali za vifo yaliyoripotiwa Jan – Machi, 2014
yalikuwa 58 wakati kipindi cha Jan-Machi, 2013 yaliripotiwa matukio 65 hivyo kuna pungufu ya matukio 7 sawa na asilimia 11.
Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi
amesema Watu waliokufa kipindi cha Jan-Machi,
2014 walikuwa 61 wakati Jan –Machi, 2013 walikuwa 81 hivyo kuna pungufu ya watu 20, sawa
na asilimia 7 huku Watu
waliojeruhiwa kipindi cha Jan – Machi, 2014 wakiwa
104
wakati Jan – Machi, 2013 walikuwa
ni 91
hivyo kufanya kuwepo kwa na ongezeko
la watu 13, sawa na asilimia 14.
Pia Katika kipindi cha Jan – Machi, 2014, jumla ya makosa 12,422 ya ukiukwaji wa
sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo la Tshs 332,790,000/= ikilinganishwa
na tozo la Tshs 365,400,000/= iliyokusanywa
katika kipindi Jan – Machi, 2013 kutokana na makosa 14,219, hivyo kuna pungufu
la kiasi cha Tshs 32,610,000/= sawa na asilimia9.
MATUKIO YA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI CHA
JAN-MACHI, 2014 NA JAN – MACHI, 2013.asilimia 9.
MATUKIO
|
12,250
|
14,375
|
-2,125
|
-15
|
MATUKIO YA AJALI
|
98
|
156
|
-58
|
-37
|
AJALI ZA VIFO
|
58
|
65
|
-7
|
-11
|
WALIOKUFA
|
61
|
81
|
-20
|
-7
|
WALIOJERUHIWA.
|
104
|
91
|
+13
|
+14
|
AJALI ZA MAJERUHI
|
40
|
91
|
-51
|
-56
|
MAKOSA YA UKIUKWAJI WA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI
|
12,422
|
14,219
|
-1,797
|
-13
|
TOZO [NOTIFICATION]
|
332,790,000/=
|
365,400,000/=
|
-32,610,000/=
|
-9
|
Mwisho.
Post a Comment