Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akitia saini kitabu cha maombolezo. |
Kandoro akiwafaliji wafiwa |
Spika Anne Makinda akiteta jambo na Waziri Hawa Ghasia ambapo katika mazishi hayo waziri ghasia amemuwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda |
Picha stori kwa hisani ya Francis Godwin Blog
Na Mwandishi wetu,Iringa
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Hawa Ghasia leo amemwakilisha waziri mkuu
Mizengo Pinda katika mazishi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo
mkoani Rukwa Marehemu Moshi Chang'a.
Katika mazishi hayo yalihudhuriwa na mamia ya
wakazi wa Manispaa ya Iringa na viongozi wa serikali
kutoka mikoa mikoa mbali mbali nchini pia spika wa
bunge Anne Makinda alitumia nafasi hiyo kuueleza umma siri
nzito iliyofichika dhidi yake ya marehemu Chang'a mwaka 1995 wakati
wa uchaguzi mkuu wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi kuwa bila
marehemu huyo asingeweza kuwa mbunge kutokana na kubanwa na chama cha upinzani
cha NCCR Mageuzi kwa kipindi hicho
Akizungumza wakati wa kutoa salama mbali mbali
kwa viongozi mjini Iringa Spika Makinda amesema
kuwa kwa mara ya kwanza mwaka 1995 alibanwa kupita kiasi
na NCCR Mageuzi katika jimbo lake la uchaguzi la Njombe kusini
na kuwa bila marehemu huyo ambae kwa kipindi hicho
alikuwa ni katibu wa CCM wilaya ya Njombe kamwe asingeweza kuwa mbunge .
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas
Kandoro akimuelezea Chang'a wakati wa kutoa salam
hizo amesema kuwa kamwe hata sahau utendaji kazi
wa mkuu huyo wa wilaya ambae amepata kufanya nae kazi katika
wilaya ya Makete ambapo yeye akiwa mkurugenzi Chang'a alikuwa ni kiongozi
wa CCM wilaya hiyo na baada ya kwenda Mbeya pia
Chang'a amefanya kazi kama mkuu wa wilaya katika mkoa huo .
Kandoro amesema kuwa utendaji kazi na utumishi uliotukuka
wa Chang'a ni mfano wa kuigwa kwa watumishi wengine wa umma
katika Taifa hili.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma amesema
kuwa mkoa wa Iringa umepata pigo kubwa kwa kifo cha
mkuu huyo wa wilaya hasa ukizingatia mchango mkubwa wa kimaendeleo
ambao amepata kuonyesha ndani ya mkoa na nje ya mkoa na kuwa kamwe mkoa
utaenzi yote aliyoyaacha .
Mkuu wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya amesema
kuwa mkoa wake amempoteza kiongozi mzalendo na aliyependa
kazi yake na kuwa hata akiwa safarini hakuwa na shaka na utendaji
kazi wa mkuu huyo wa wilaya na kuwa siku zote mbali ya
kuongoza kama kiongozi wa serikali ila wakati mwingi alitumia kuwahubiria
upendo wananchi wa wilaya yake.
Kwani alisema kuwa alikuwa hawezi kuanza mkutano bila
kumhubiri mwenyezi Mungu mbali ya kuwa yeye alikuwa muumini wa dini
ya Kiislam ila alikuwa akihubiria dini ya kikristo .
Hata hivyo amesema kuwa hadi kesho anaamini
alishinda ubunge jimbo hilo mwaka 1995 si kwa uwezo wake
bali alishinda kwa uwezo wa marehemu Chang'a ambao alionyesha
uwezo mkubwa wa kumnadi na hata kufanikiwa kuwa mbunge wa
jimbo hilo na leo kuwa spika wa bunge .
Viongozi wengine waliopata kushiriki katika mazishi hayo
ni pamoja na viongozi msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya
siasa Ikulu Rajab Luhwavi pia viongozi kutoka mkoa wa Mwanza , Singida
,wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano akiwemo mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na Lediana Mafulu (CCM)
naibu waziri wa maliasili na utalii Mahamudu Mgimwa ambae pia ni
mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin,baadhi ya wajumbe wa bunge la
katiba kutoka mkoa wa Iringa na wakuu wa wilaya mbali mbali akiwemo
mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamwoto mkuu wa wilaya ya Iringa Dr
Letisia Warioba ,mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita na
wengine wengi
mwisho
Post a Comment