Mmoja wa wajumbe akichangia maada katika kikao hicho |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais,
anayeshughulikia utawala bora, George Mkuchika, amesema vitendo vya
watendaji wa halmashauri kujiuhusisha na wizi wa fedha za miradi ya maendeleo
kumetokana na Madiwani kushindwa kutambua majukumu yao.
Waziri Mkuchika am,esema hayo jijini Mbeya wakati
akizungumzia suala la utawala bora na rushwa jinsi zinavyoathiri utekelezaji wa
miradi ya maendeleo, katika kikao cha kamati ya ushari ya Mkoa (Rcc) Mbeya.
Amesema, Madiwani wamekuwa hawatambui wajibu wao
katika kusimamia fedha zote za miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa tenda
mbalimbali kwenye halmashauri zao hivyo kutoa mianya ya rushwa kwa
watendaji.
Amesema, endapo vitendo hivyo havitasimamiwa au
kudhibitiwa , Taifa halitaweza kuwa na maendeleo endelevu ya kijamii na
kiuchumi.
Akizungumzia suala la vitendo vya rushwa , amesema
katika matukio 288 yaliyolipotiwa katika Taasisi ya Kuzuia na kupambana na
rushwa nchini (Takukuru) kwa mkoa wa Mbeya, halmashauri ndizo
ziliongoza kwa kuwa na jumla ya tuhuma 65.
Amezitaja sekta nyingine kuwa ni Mahakama kuwa tuhuma
(46), polisi (35), sekta binafsi (35), huku serikali Kuu, uhamiaji, Maliasili,
Taasisi za dini, Jeshi la wananchi (JWTZ) na vyombo vya habari zikiwa na jumla
ya tuhuma moja tu kila mojawapo.
Aidha, Mkuchika amezitaka halmashauri zote nchini
kuandaa utaratibu wa kuwaita na kuwashirikisha Takukuru katika vikao vyao
vya kujadili masuala ya maendeleo .
Akizungumzia vitendo vya Rushwa , Mkuu wa Takukuru
Mkoa wa Mbeya, Felix Wandwe, alisema licha a kushughulikia rushwa ndogo
ndogo TAKUKURU pia imeendelea na uchunguzi wa kuendesha kesi za rushwa
kubwa mahakamani.
Hata hivyo amebainisha kuwa kwa Mkoa wa Mbeya kuanzia mwezi Januari hadi
Desember 2013 jumla ya matukio ya rushwa 288 yaliyolipotiwa katika
taasisi hiyo huku majalada 42 yakiwa tayari yamechunguzwa na kukamilika.
Post a Comment