KEROOO YANGU……..
Mimi naitwa Josephat
Mwokozi Mkazi wa Isanga Jijini Mbeya
kero yangu kubwa ni Kuhusu Hospital ya Mkoa wa Mbeya kwakweli Hospital hii
imekuwa na shida sana kama hunapesa huwezi pata matibabu na asilimia ya
kupoteza maisha ni kubwa sana,Kuna baadhi ya madaktari wapo kwa ajili ya rushwa tu awana
kazi ya kufanya nimeshudia juzi tu Ndugu Mwandishi Mama Mjamzito kidogo apoteze
maisha yake kwasababu madaktari wa zamu kitengo cha upasuaji walitaka kupatiwa
kiasi cha shilingi laki moja ili mama huyo akafanyiwe upasuaji na huku
mama huyo yako katika hali mbaya bahati
nzuri ndugu mwandishi familia ya mama huyo walikusanya kiasi cha shilingi elfu
60 sasa sijui kama mama huyo alipona au laaa,,,,kwa kweli tumepiga kelele
tumechoka tumemuachia mungu tu atuponye maana sisi maskini ndo tupoteza maisha
,,,,,,,,,,,chonde chonde usipunguze wala kuongeza chochote kwenye hilo suala naomba ujume ufike……..Mungu
Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika,,,,,,,,Pamoja tulijenge taifa letu,,,,,,
Post a Comment