Mita ikonyesha kuisha kwa Luku huku umeme ukiendelea kutumika na katika karakana hiyo. |
Upekuzi ukiendelea kubaini mbinu na janja janja za wizi wa umeme |
Polisi haamini macho yake mara baada ya kuvamia moja eneo linalotuhumiwa kuhiska na wizi wa Umeme katika eneo la Ilomba jijini mbeya . |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Shirika la Umeme Tanesco Mkoani
Mbeya bado linakabiliwa na Tatizo la kuwepo kwa mafundi umeme feki wa mitaani
ambao wamekuwa wakiunganishia wananchi huduma hiyo hali ambayo imelifanya
shirika hilo kuingia hasara kubwa.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kuwepo
kwa msako unafanywa na shirika hilo Mkoani Mbeya na maeneo mengine kwa ujumla
kwa lengo la kubaini watu wanaolihujumu shirika hilo.
Afisa Usalama mwandamizi wa shirika
hilo kwa Mkoa wa Mbeya Ndugu Siprian Lugazia amesema vitendo vya kuliibia
shirika kwa kujiungnishia umeme majumbani vimeanza kuibuka upya katika kipindi
cha kuanzia mwezi January hadi Aprily mwaka uu kwa baadhi ya maeneo mkoani
humo.
Lugazia amedai kuwa wamekuwa wakipata taarifa mbalimbali toka kwa
baadhi ya wananchi juu ya kuwepo kwa vitendo hivyo.
Amesema mara baada ya kufuatilia
taarifa hizo walibaini kuwepo kwa hali hiyo kwa baadhi ya wateja wao ambao hata
hivyo baadhii yao walikili kufanya udanganyifu huo huku baadhi yao
wakidai kuunganishiwa na mafundi wa mitaani .
Hata hivyo amefafanua kuwa hivi
karibuni wamekamata mmoja wa wajasilimali wanaojihusisha na uchomeleaji katika
eneo la Ilomba jijini mbeya na kumchukulia hatua za kisheria
Hata hivyo Afisa huyo amesema msako
huo utaendelea kufanyika mara kwa mara kwa lengo la kukomesha kabisa vitendo
hivyo
Post a Comment