Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Na EmanuelMadafa,Mbeya.

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limefanikiwa kuzima vurugu zilizotaka kutokea katika baadhi ya maeneo hususani eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya

Vurugu hizo zilitaka kutokea kutokana  na baadhi ya wafanyabiashara Ndogondogo Machinga jijini humo kwa madai kuwa wamekosa maeneo ya kufanyia biashara hasa mara baada ya Halmashauri ya jiji la mbeya kuwaondoa wafanyabiashara hao Machi 12 mwaka huu.
Agizo hilo la kuwaondoa wafanyabishara nikuwataka wafanyabiashara kuondoka  katika maneno ambayo hayakutakiwa kufanyiwa biashara kandokando ya barabara ya Dar es salaam ,Tunduma ambayo hata hivyo wengi wa wamachinga hao wametii agizo hilo.
 .
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara hao wamedai kuwa  vurugu hizo zilitaka kutokea kutokana na baadhi yao kudai kukosa maeneo ya kufanyia biashara mara baada ya kuhamishwa mahali walipokuwa awali.
 
Hata wafanyabiashara hao waliamua kupiga mawe geti katika soko jipya la Mwanjelwa kwa lengo la kutaka kufanyia biashara ndani ya soko hilo pamoja na kupanga mawe barabarani hali ambayo iliwalazimu jeshi la polis kutumia nguvu na kuwatanya wafanyabiasahra hao.

Pia kutokana na hali hiyo hofu kwa baadhi ya wafanyabiashara ilitanda katika eneo la Mwanjelwa ambapo walilazimika kufunga maduka yao kwa kuhofia vurugu kutokea kwa zaidi ya masaa kadhaa ambapo baadae maduka hayo yalifunguliwa na baishara kuendelea kama kawaida mara baada ya jeshi la polisi kuingilia kati nakuzima hali hiyo.







picha na Jamiimoja.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top