Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kocha wa Taifa Stars Cha Maboresho kilicho weka kambi Mjini Tukuyu Mbeya Oscar Koloso akizungumzia juu ya maendeleo ya kikosi hicho.

Na EmanuelMadafa,Mbeya

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Maboresho  ya Taifa Stars Ndugu Oscar Koloso ameomyesha kuridhishwa na kiwango cha wachezaji walioteuliwa kujiunga na Kambi ya mwezi mmojaWilayani Rungwe  Tukuyu Mbeya .

Vijana hao 33 wameweka kambi  wilayani humo  Katika Hotel ya LandMark Hotel kwa lengo la kupatiwa mafunzo na hatimaye  kupata  vijana 15 watakao jiunga na Timu ya Taifa .

Akizungumza katika uwanja wa Mazoezi katika Chuo Cha Ualimu Cha Msasani kilichopo Wilayani humo Kocha Koloso amesema kuwa kwa sasa vijana hao wapo katika hali nzuri licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo ambazo wameweza kukabiliana nazo.

 Amesema kwa asilimia kubwa vijana hao wameonyesha uwezo mkubwa katika kufanya mazoezi pamoja na kuonyesha ushirikiano mzuri kwa makocha wao licha ya baadhi yao kutatizwa na hali ya hewa yenya baridi na mvua za hapa na pale..

Hata hivyo Kocha huyo ameeleza kuwa na  wasiwasi juu ya muda waliopewa kambini kwa ajili ya kuanda timu bora ambayo itaweza kuleta mabadiliko katika timu ya Taifa.

Amesema nivyema viongozi wa TFF wakajaribu kuangalia utaratibu wa kuongeza muda zaidi kwenye mafunzo hayo  kwa lengo la kufikia malengo yaliyokusudiwa na TFF.

Amesema  kutokana na kuwepo kwa muda mchache kambini hapo wamejaribu kufupisha baadhi ya mazoezi ili kuendana na muda uliowekwa na TTF ambao ni mwezi mmoja tu.

Kutokana na hali hiyo Kocha huyo amewataka wadau mbalimbali pamoja wananchi kwa ujumla kukipa muda zaidi kikosi hicho ili kiweze kufanya vizuri kwa kipindi cha baadae ambacho kinatalajiwa na wengi.

Pamoja na hali hiyo Koloso amesema  kwa sasa wapo vizuri kimchezo kwa ajili ya kupambana na Timu ya Taifa ya Malawi itakayo chezwa hivi karibuni katika uwanja wa sokoine jijini Mbeya.
Mwisho.


Picha na Jamiimojablog.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top