Na EmanuelMadafa,Mbeya
UMLA ya shilingi milioni
34,070,000 zimepatikana katika mechi ya Mbeya City na Azam ya Jijini Dare es salaam
iliyochezwa April 13 mwaka huu katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine huku
timu ya Azam ikiondoka na Ushindi kiduchu wa wa goli 2-1.
Akisoma mapato hayo Katibu wa chama
cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) Selemani Harubu , amesema kati mapato
hayo shilingi milioni 7,628,074.99 zimeenda kwa kila timu.
Amesema, gharama ya Vat ni shilingi
milioni 5,197.118.64 tiketi shilingi 3,015,000 gharama ya mchezo 2,327,209,305.32huku
kamati ya ligi ikiondoka na shilingi 2,327,209.322.
Amesema, TFF imepata
shilingi 1,163,604.66 na MREFA ikiondoka na shilingi 905,025,84 na uwanja
ukipata shilingi 3,878,682.20.
Aidha katika Mchezo baadhi ya wadau
mbalimbali wa mpira jijini mbeya wamedai kuwa ushindi huo wa Azam hakuwa sawa
kwa madai kuwa mwamuzi wa mchezo huo Nathan Lazaro kutoka Kilimanjalo kuwa
aliipa ushindi Azam kwa goli lisilo halali .
Aidha kufuatia matokeo hayo Azam
wamejitawaza kuwa mabingwa wapya ligi kuu vodacom Tanzania Bara kwa kufikisha
Pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote huku ikibakiwa na mchezo
mmoja mkononi .
Mwisho..
Post a Comment