David Mwamaja Kocha Tanzania Prisons |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
KOCHA wa Timu ya Tanzania Prisons David
Mwamaja, amesema mshikamano na upendo kwa wachezaji wake ndio siri kubwa
iliyoiwezesha timu hiyo kuvuka kizingiti cha kutokushuka daraja.
Amesema, licha ya timu yake kushindwa
kufanya vizuri kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania yaliyomalizika
April 19 mwaka huu lakini amejivunia nidhamu ya wachezaji wake
waliyoionesha pindi wakiwa kambini na uwanjani.
Akizungumza na Blog hii Mwamaja
amesema:” Mara tu alipokabidhiwa kuinoa timu hiyo kwenye mzunguko wa pili
baada ya kuondolewa kwa kocha Jumanne Charles kitu cha kwanza alichokifanya ni
kuwajenga wachezaji kisaikolojia
kwa kuwa na umoja, mshikamano na upendo.
Amesema, timu hiyo imebahatika kwa kuwa na
wachezaji wazuri ambapo hakusita kumpongeza kocha Jumanne na viongozi wengine
kujitahidi kusajili wachezaji wazuri tatizo lililokuwepo lilikuwa ni kukosekana
kwa hali ya umoja na mshikamano kwa wachezaji hivyo baadhi yao walikatatamaa.
Aidha, kocha Mwamaja aliwashukuru
mashabiki na wadau wa mpira wa Mkoa wa Mbeya kwa ushirikiano waliouonesha
katika kipindi chote kigumu cha kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja.
katika mashindano mambo mengi
hujitokeza yapo yatakayowapendeza mashabiki na wadau na yale yatakayowachukuza
hivyo ni vema yakamalizika kwa kuombana msamaha na kuangalia mchakato
ujao.
Timu hiyo imewesza kubaki katika mashindano ya ligi kuu kwa kuwa na pointi 28
Mwisho.
Post a Comment