Afisa Mahusiano Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya Ndugu Neema Stanton akifafanua jambo |
Na
EmanuelMadafa,Mbeya
Mamlaka ya
maji safi na Usafi wa Mazingira Uwsa jijini Mbeya imeendelea kukumbana na
changamoto ya kuwepo mafundi feki (Vishoka)ambao wamekuwa wakiunganishia watu
maji .
Akizungumzia
hali hiyo Afisa Mahusiano wa Mamlaka hiyo Ndugu Neema Stanton amesema kuwa
kumeibuka kwa wimbi la watu ambao si watumishi wa mamlaka hiyo ambao wamekuwa wakiunganishi watu maji na kwa
kuwatoza fedha kidogo kama sehemu ya malipo ya kazi hiyo.
Amesema hali
hiyo imebainika mara baada ya mamlaka hiyo kuanza msako kwa nyumba hadi
nyumba kwa lengo la kukata maji kwa
wadaiwa sugu .
Amesema Katika
msako baadhi yao walibainika kutumia huduma hiyo ya maji pasipo kuwa na akaunti
ya kulipia huduma hizo za maji kama taratibu zinavyo taka.
K wa mujibu
wa Afisa Mahusiano huyo mafundi hao vishoka wamekuwa wakichukua fedha kidogo na
kuwaunganishia watu maji pamoja na
baadhi yao kuto pata kabisa huduma hiyo licha ya kutoa fedha.
Post a Comment